Mratibu wa Miss KIgamboni 2012, Somoe Ng'itu kushoto akiwa na Mkurugenzi wa K&L, Angela Msangi, Miss Kigamboni namba mbili, Agness Goodluck na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigamboni asubuhi hii |
Somoe akisaini kitabu cha wageni katika shule hiyo |
Angela akisaini kitabu cha wageni katika shule hiyo |
Mwanafunzi Sebastian akishukuru |
Makabidhiano |
Makabidhiano |
Makabidhiano |
Agness akisaini kitabu cha wageni |
Na Princess Asia
WAANDAAJI wa Miss Kigamboni 2012, K&L Media Solutions,
asubuhi ya leo wamekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5
kwa uongozi wa Shule ya Msingi Kigamboni, ikiwa ni kutimiza ahadi yao ya kuchangia
sehemu ya pato kutokana na shindano lao, lililofanyika Juni 15, mwaka huu katika
ukumbi wa Navy Beach, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akikabidhi vifaa hivyo, katika shule hiyo iliyopo mkabala na
Mahakama ya Mwanzo ya Kigamboni, Mratibu wa Miss Kigamboni 2012, Somoe Ng’itu alisema
kwamba waliahidi kufanya hivyo kwa sababu wanajua umuhimu wa elimu na
wanathamini na pia baadhi ya waandajii na warembo wa shindano hilo, walisoma
katika shule hiyo.
Somoe, ambaye pia ni Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi
wa gazeti la Nipashe, alisema kwamba kampuni yao imeamua pia kufanya hivyo ili
kutoa mfano kwa wadau wengine kuchangia miradi ya maendeleo ya elimu.
Aidha, Somoe ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), alisema kwamba kutimiza ahadi
hiyo ni mwanzo tu kwao wa kufanya mambo mengi mengine katika kuchangia miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Akipokea misaada hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Colombani
Mpogola alisema anawashukuru sana K&L Media Solutions kwa msaada huo, kwani
umekuja katika wakati mwafaka na mara moja umeanza kufanyiwa kazi kwa
kukarabati baadhi ya madarasa ya shule hiyo.
Mwalimu Mpogola alisema kwamba K&L wametoa mfano mzuri
na akawataka wadau na makampuni mengine kuiga mfano huo.
Mwanafunzi wa darasa la saba, Sebastian Charles alishukuru
kwa niaba ya wanafunzi wenzake naye pia akatoa wito kwa wadau wengine kuiga
mfano huo. Katika shindano la Miss Kigamboni lililofana Juni 15, mwanafunzi wa
mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Eddah Sylvester (21) aliibuka
mshindi, wakati Agnes Goodluck (20), anayesoma Chuo cha Usimaizi wa Fedha (IFM)
mwaka wa pili aliibuka mshindi wa pili na Elizabeth Boniphace (21) aliibuka wa
tatu.
Washindi hao watatu, na wengine wawili walioingia tano bora,
Esther Albert (19) na Khadija Kombo (21) watashiriki shindano la Miss Temeke, Septemba
mwaka huu kusaka tiketi ya kushiriki Miss Tanzania Novemba, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment