Martine Sospeter |
Na Princess Asia
BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanakibega' Jumapili hii itaanza
bonanza maalum katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam, ambako mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC wameweka kambi yao ya mazoezi kwa sasa.
Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter,
alisema kuwa kwa kuanzia Jumapili hii ya Julai mosi itakuwa ikifanya maonesho
yake uwanjani hapo.
Sopeter alisema kuwa bendi hiyo itakuwa na bonanza lake
maalum ambalo linajulikana kama (Mashujaa Sunday Soccer Bonanza) itakayokuwa
ikifanyika hapo kila Jumapili.
Alisema burudani kutoka kwa bendi hiyo itaanza saa 9.Alasiri
na kumalizika saa 3,usiku.
"Tumejipanga kuwapa wakati wa temeke burudani ndiyo
maana tumeamua kuleta burudani hiyo kila Jumapili na itakuwa ikifanya maonyesho
yake kwa zaidi ya masaa saba ili kila mmoja aweze kuridhika na onesho
letu"alisema Sospeter.
Alisema bendi hiyo chini ya Rais Chalz Baba imejipanga
kuhakikisha inatoa burudani mwanzo mwisho na kuridhisha wapenzi wao.
0 comments:
Post a Comment