Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya


MAN UNITED YAIKOMOA CHELSEA USAJILI WA BEKI LA KIBRZIL...


KLABU ya Manchester United inajipanga kumuongezea mkataba mpya Rafael da Silva, mwenye umri wa miaka 21, ili kuwakata maini wapinzani wao katika Ligi Kuu England, Chelsea wanaommezea mate beki huyo Mbrazil.
Dimitar Berbatov
Berbatov 
KLABU ya Malaga inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, baada ya kuelezwa kwamba atatemwa na klabu yake.
MSHAMBULIAJI wa Croatia, Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 26, ameiambia Everton kwamba watalazimika kusubiri hadi mwishoni mwa Euro 2012 kabla ya kutatua mustakabali wake.
KLABU ya Manchester City itatakiwa kulipa kiasi cha pauni Milioni 30 ili kumnasa mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente, mwenyr umri wa miaka 27.
KINDA wa Manchester United, Zeki Fryers, mwenye umri wa miaka 19, anaweza kuondoka Old Trafford, na klabu za Tottenham, Newcastle na Burnley zote zikiwa tayari kumsajili beki huyo wa kushoto.
KLABU ya Reading iko tayari kumuongezea mshahara Pavel Pogrebnyak, mwenye umri wa miaka 28, ili iwe naye. The Royals wametoa ofa ya pauni Milioni 13 kwa mshambuliaji huyo.
Nicklas Bendtner
Nicklas Bendtner 
KLABU ya Benfica iko tayari kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, baada ya mshambuliaji huyo kung'ara dhidi ya Ureno.
KLABU ya Chelsea imepanga kukata pauni Milioni 10 ili kumnasa winga wa Wigan, Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21.

MABOSI WATATU WASIMAMISHWA CHELSEA
MAOFISA watatu wa klabu ya Chelsea wamesimamishwa baada ya taji la Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kupata hitilafu.
BEKI wa Bolton, Zat Knight, mwenye umri wa miaka 32, anajiandaa kusaini mkataba mpya Uwanja wa Reebok, licha ya kwamba wameshuka daraja kutoka Ligi Kuu.
NYOTA wa Chelsea, Juan Mata amesema kwamba klabu yake imemruhusu kuchezea Hispania katika kikosi cha Olimpiki.

VAN PERSIE, BENT KUIGIZA...

WASHAMBULIAJI wa Ligi Kuu ya England, Robin van Persie na Darren Bent wanatarajiwa kutokea katika mfululizo wa vipindi vya Televisheni ya ITV, viitwavyo Red Or Black.