Van Persie |
Mabingwa hao wa Ligi Kuu England wameonyesha nia ya kumsajili mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Uholanzi, lakini si kwa dau zaidi ya hilo.
MWANAUME VAN | |
REKODI YA VAN PERSIE 2011-12 ARSENAL | |
MECHI MABAO PASI ZA MABAO | 51(3) 40 9 |
Chanzo kimoja cha habari na cha karibu kimesema: “Kiwano hicho hakiwezi kuongezwa na City. Hawako tayari kutoa zaidi ya pauni Milioni 15 ili wampe mshahara mnono.”
City inataka kumpa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki Van Persie kuhamishia huduma zake Uwanuja wa Etihad.
Hata kama City itafanikiwa kuwauza wachezaji wake Emmanuel Adebayor, Roque Santa Cruz, Wayne Bridge na Kolo Toure kwa dau zuri, lakini bado haitakuwa tayari kumnunua Nahodha wa Arsenal kwa zaidi ya kiasi hicho.
Kocha Roberto Mancini yuko tayari kuachana na mchezaji huyo na kuhamishia mawindo yake kwa mshambuliaji wa Napoli,Edinson Cavani, kama Arsenal haitakuwa tayari kumuuza kwa bei wanayotaka.
Van Persie, ambaye anatarajiwa kwenda kujipumzisha na familia yake baada ya Uholoanzi kutolewa kwenye Euro 2012, amegoma kuongeza mkataba wake Arsenal, ambao unatarajiwa kumalizika mwakani.
0 comments:
Post a Comment