Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


NYOTA WA LA LIGA AOTA MBAWA MAN UNITED, MAN CITY...

KLABU za Manchester United na Manchester City zinaelekea kumkosa nyota wa Athletic Bilbao, Javi Martinez, mwenye umri wa miaka 23, ambaye anakaribia kujiunga na Bayern Munich.
Javi Martinez
Javi Martinez 
KIUNGO Luka Modric anataka Tottenham wakala wake amemuambia Mwenyekiti Daniel Levy inawezekana ikawa wiki ijayo. Manchester United, Real Madrid na Paris St-Germain zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kumchukua kiungo huyo wa Croatia.
KLABU ya Manchester United inajipanga kumchukua beki wa pembeni wa PSV Eindhoven, Jetro Willems,  mwenye umri wa miaka 18, baada ya kumfuatilia wakati wa Euro 2012 akiwa na kikosi cha Uholanzi.
KLABU za Chelsea, Tottenham na Liverpool zinapigana vikumbo kuwania saini ya mshambuliaji wa Malaga na mwanasoka wa kimataifa wa Venezuela, Salomon Rondon,  mwenye umri wa miaka 22.
KLABU ya Everton inataka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Luc Castaignos.  Kinda huyo wa miaka 19 amecheza mechi sita tu katika kikosi cha timu hiyo ya Italia, tangu aondoke Feyenoord mwaka 2011.
KOCHA mpya wa Swansea, Michael Laudrup anataka mchezaji wake wa kwanza kununua awe nyota wa kikosi cha Denmark, Euro 2012, Michael Krohn-Dehli,  mwenye umri wa miaka 29, kutoka Brondby.
KLABU ya Manchester City iko tayari kumalizana na mshambuliaji wa timu iliyotolewa mapema kwenye Euro 2012, Robin van Persie.
BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, ataipiga chini ofa ya Manchester City kama atahakikishiwa na kocha mpya, Brendan Rodgers kwamba Wekundu hao watatimiza matarajio yake.
Michael Krohn-Dehli
Michael Krohn-Dehli
KIUNGO wa Roma, Mtaliano Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 28, ameiweka mkao wa kula Manchester City kwa kueleza nia yake ya kucheza Ligi Kuu ya England.
KOCHA wa Stoke, Tony Pulis anataka kumsajili wimga wa Wolves, Matt Jarvis.

OWEN KUWA KOCHA

KIUNGO Owen Hargreaves atakuwa mchezaji mwingine wa England aliyestaafu na kuingia kwenye ukocha hivi karibuni.
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas anajiamini atatajwa kuwa kocha mpya wa Tottenham, wakati klabu hiyo ikitarajiwa kumtaja mrithi wa Harry Redknapp wiki ijayo.
KIPA wa Tottenham, Carlo Cudicini amepokea kwa moyo mkunjufu wazo la klabu yake kujzungumza na kocha wa zamani wa Chelsea, Ande Villas-Boas ili arithi mikoba ya Harry Redknapp Uwanja wa White Hart Lane.
MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi wa klabu ya Barcelona ya Hispania, amesema kwamba siku ambayo atastaafu ndio atamaliza mambo yote.

WACHEZAJI ENGLAND WAAHIDIWA 'FEDHA CHAFU'

CHAMA cha Soka England, kitabomoa benki na kutoa pauni Milioni 20 kama kikosi chao cha England kitatwaa taji la Euro 2012, lakini kocha Roy Hodgson amesema: "Sishobokei fedha, ni medali."
KOCHA Roy Hodgson atawaambia wachezaji wake hawatakiwi kuiogopa Italia na kupoteza kujiamini watakapokutana na mabingwa hao wa Kombe la Dunia mara nne kwa sababu ya wasifu wao na historia yao, katika Robo Fainali ya Euro 2012 Jumapili.
BEKI Alvaro Arbeloa amejibu kejeli kwamba kikosi cha Hispania kinaboa. Habari kamili: the Guardian