Katibu Mkuu wa Ndani sport Club Jarahi Kilemile Akizungumza na wanamichezo na Watumishi Raia wa wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi baada ya kumchagua kuwa Katibu Mkuu wa Klabu hiyo.
KLABU ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Ndani Sports Club) imefanikiwa kupata Viongozi wake katika uchaguzi uliofanyika baada ya uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake.
Viongozi waliochaguliwa ni Pamoja na Mwenyekiti Juma Katanga kutoka Idara ya wakimbizi, Katibu mkuu ni Jarahi Kilemile kutoka Idara ya Polisi na Mweka Hazina Daniel Njau kutoka idara ya Utawala ya mambo ya Ndani ya Nchi.
Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Uongozi wa TUGHE pia uliwachagua Viongozi watakao iwakilisha wizara kwenye SHIMIWI na Wajumbe wa Kamati Kuu ambapo idara zote zilishiriki.
Akiongea baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti Juma Katanga alisema atahakikisha anatumia Michezo kuitangaza wizara hiyo nakuhakikisha Timu za Wizara hiyo zinafanya vizuri katika Michezo yote watakayo shiriki.
Naye Katibu Mkuu Jarahi Kilemile alisema Michezo katika wizara ya Mambo ya Ndani ni muhimu na watumishi na wanamichezo wa wizara hiyo watarajie uwakilishi mzuri na wenye kuleta mafanikio.
“Nitahakikisha timu zetu zinafanya vizuri na kila mtumishi anayehitaji kushiriki michezo anapata fursa hiyo kwakuwa michezo ni afya na lengo nikuhakikisha tunakuwa na timu imara ambayo haisumbuliwi na wizara nyingine yeyote”Alisema Kilemire.
Klabu hiyo inaundwa na watumishi raia na wanamichezo kutoka Idara ya Polisi, Magereza,Uhamiaji,Wakimbizi, NIDA pamoja idara ya Utawala ya wizara hiyo
0 comments:
Post a Comment