Thomas Ulimwengu, mshambuliaji wa Ngorongoro |
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda
kabla ya kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba Ngorongoro
Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob Michelsen
itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai 3 na 5 mwaka
huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
Amesema mechi zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo
Ngorongoro Heroes, Misri na Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka
tiketi za kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20
zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
Katika raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan
ambapo katika raundi ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika
jijini Dar es Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili
baadaye nchini Nigeria.
Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi
ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment