Hitima Yanga imekwishasomwa, iliongozwa na Sheikh Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili
Imani Omar Madega, Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa Julai
15, Clement Sanga walikuwapo. Sasa watu wanakula, BIN ZUBEIRY anaondoka
eneo la tukio.
|
Waungwana baada ya kisomo wakisubiri sadaka |
|
Sheikh Mussa kulia, kushoto ni Katibu wake Almasi lailly Mussa na nyuma yao ni mwanachama wa Yanga, Mustafa Mohamed, Katibu wa Tawi la Kurasini |
|
Madega kulia, akiwa na Sanga kushoto kwake |
|
Waungwana wakisubiri sadaka baada ya dua |
|
Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kulia, Madega na Sanga |
|
Sheikh Mussa katikati, kulia Juma Mnonji mwanachama wa Simba, na kushoto Katibu wake, Almasi |
|
Waungwana baada ya dua wakisubiri sadaka |
Maandalizi ya hitima katika klabu ya Yanga, makao makuu wa
klabu, makutano ya mitaa ya twiga na Jangwani yanaendelea muda huu. Mboga
zinakaribia kuiva, mchele umekwishaanza kuoshwa. Ng’ombe wawili wako jikoni. Ibada
ya hitima yenyewe inakaribia kuanza kusomwa.
|
Akina mama wakichambua mchele |
|
Akina mama wakichambua mchele |
|
Eneo la kusomea ibada ya hitima |
|
Waungwana tayari kwa kisomo cha hitima |
|
Mwanachama maarufu wa Simba, Mzee Juma Mnonji wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye hitima kama mmoja wa wageni waalikwa |
|
Masufuria jikoni |
|
Jamaa anatengeneza viungo |
|
Ng'ombe anaiva |
0 comments:
Post a Comment