|
Lisa katikati akiwa na wenzake |
Na Princess Asia
KIMWANA Lisa Jensen usiku huu ameibuka kinara katika
shindano maalum la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katka shindano la Miss World
mwaka huu, lililofanyika kwenye ukumbi wa 327, Mikocheni, Dar es Salaam.
Shindano hilo, lililoshirikisha washiriki wa zamani wa Miss
Tanzania ambao hawajawahi kushinda, dalili za Lisa kushinda zilionekana tangu mwanzo,
kutokana na kuwafunika washiriki ‘ile mbayaaa’ washiriki wenzake tisa.
Shindano hilo, lilianzia kwa warembo kucheza shoo ya
ufunguzi kama ilivyo ada ya mashindano ya Miss Tanzania, baadaye wakapita na
vazi la ubunifu, ufukweni na kumalizia na vazi la jioni, ambako kote Miss Mara
wa 2006 alifunika mbaya.
Aliyemfuatia Lisa ni Hamisa Hassan kutoka Kinondoni, wakati
mshindi wa tatu alikuwa ni Pendo Laiser Miss Arusha 2008 na wengine walioingia
tano bora ni Stella Mbuge na Jennifer Kakolaki.
Washiriki wengine ni Glorybayanca Mayowa, Queen Issa,
Christine William, Mwajabu Juma na Neema Saleh.
Shindano hili, linafanyika kufuatia kalenda ya mashindano ya
Miss Tanzania kubadilika na washindi wa mashindano ya mwaka huu ngazi ya awali
watashiriki katika shindano la Miss Tanzania baadaye mwaka huu, kumpata
mwakilishi wa Miss World mwakani.
|
Waalikwa wakifuatilia shindano |
|
Warembo shoo ya ufunguzi |
|
Lisa akipongezwa na Salha, Miss Tanzania 2011 baada ya kuvikwa taji |
|
Lissa akipunga mkono katikati |
|
Majaji wakipiga hesabu |
|
Jaji Mkuu wakitangaza top 5 |
|
Majaji kazini |
|
Waalikwa |
|
Waalikwa |
|
Majaji |
|
Jane John na kaka ake BIN ZUBEIRY |
|
Fimbo Butallah na kimwana |
|
JK akisomesha |
|
Sura za furaha |
|
Glory na rafiki zake |
|
Hizi kazi zetu hizi, we acha tu. Issa Mnally 'Duwa Chee' |
|
Prashant anatetwa mbele yake |
|
Waalikwa |
|
Top three |
|
Wataalamu |
|
Top 5 |
|
Salha anamvalisha taji Lissa |
|
Mwaaa! hongera mama, Salha akimvisha taji Lissa |
0 comments:
Post a Comment