// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LEO NI MIAKA MITANO TANGU KIFO CHA MPIGANAJI AMINA CHIFUPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LEO NI MIAKA MITANO TANGU KIFO CHA MPIGANAJI AMINA CHIFUPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 26, 2012

    LEO NI MIAKA MITANO TANGU KIFO CHA MPIGANAJI AMINA CHIFUPA


    Marehemu Amina Chifupa
    Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya.

    Amina leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena katika Redio ya Clouds FM.

    Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania wataendelea kumuenzi na  atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa dawa ya kulevya.

    Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini.

                                               Pumzika kwa Amani Amina Chifupa!

    Chini ni picha za baadhi ya matukio mbalimbali ambayo Amina chifupa aliweza kushikiriki wakati wa Uhai wake. Picha Hizi zilipigwa enzi hizo na John Badi wa Daily Mitikasi Blog
    Amina Chifupa alipenda michezo hali iliyompelekea mara kwa mara kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya michezo. Hapa ilikuwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, akikabidhi vifaa hivyo kwa Mh. Nchimbi wakati huo akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
    Amina Chifupa akiteta jambo na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Alnoor Kassum katika moja ya shughuli za kitaifa enzi za uhai wake. Hapa ilikuwa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Foundation jijini Dar.
    Siku Amina Chifupa alipokula kiapo bungeni mjini Dodoma.
    Amina (wa pili kushoto), akiwa na wabunge wenzake siku walipotembelea katika Nyumba ya Vipaji ya THT, wakati ikiwa pale Kinondoni katikati ya Biafra na Moroco.
    Amina alikuwa mpenzi wa muziki pia hapa ilikuwa wakati huo ikiitwa Sheraton Hotel kwa sasa ni Serena, Bendi ya Twanga walikuwa wakitumbuiza katika hafla moja.
    Amina alipiga vita matumizi ya dawa za kulevya na hapa alikuwa mgeni rasmi katika semina iliyotolewa kwa wanafunzi kuhusu madhara ya dawa hizo.
    Amina Chifupa alipenda sana watoto hali iliyomfanya kujikita katika utoaji wa misaada katika vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima na waliokatika mazingira magumu. Hapa ilikuwa baada ya kutoa msaada katika kituo kimoja kilichopo Sinza.
    Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Amina aliweza kuandaa futari na kukaribisha watu mbalimbali. Hapa ilkuwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar, akijadiliana jambo na Bi. Shyrose Bhanji ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEO NI MIAKA MITANO TANGU KIFO CHA MPIGANAJI AMINA CHIFUPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top