// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIMWANA WA HOLLYWOOD AJA KUSHIRIKI MOUNT MERU MARATHON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIMWANA WA HOLLYWOOD AJA KUSHIRIKI MOUNT MERU MARATHON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, June 16, 2012

    KIMWANA WA HOLLYWOOD AJA KUSHIRIKI MOUNT MERU MARATHON

    Deidre Lorenz
    Na Princess Asia
    MCHEZA sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani, Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi. 
    Ofisa Uhusiano wa Mount Meru Marathon, Grace Soka, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.
    Amesema ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight,  na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.
    Amesema Eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu  ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.
    Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.
    Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMWANA WA HOLLYWOOD AJA KUSHIRIKI MOUNT MERU MARATHON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top