Na Abdallah Jongo
VIONGOZI na wadau wa
soka wilayani Kilosa,wamekitaka chama cha soka wilayani humo KDFA kutoandaa na
kusimamia tena michuano ya copa coca
cola mwakani kwa madai ya kushindwa kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Hatua ya viongozi hao imekuja kufuatia KDFA kushindwa kugawa
vifaa vinavyotolewa na mdhamini wa michuano hiyo na kuisafirisha timu ya wilaya
ya Copa Coca Cola kwenda kushiriki michuano hiyo ngazi ya mkoa
Wakizungumza na gazeti hili,viongozi na wadau hao wamesema
kuwa kitendo kilichofanywa na KDFA cha kushindwa kuisafirisha timu iliyoteuliwa
katika michuano ya copa coca cola kimewasikitisha na kudai kuwa hali hiyo
itachangia kudumaza maendeleo ya soka kwa kushusha morali na kuwanyima fursa
wachezaji chipukizi walioibuliwa katika michuano hiyo.
Aidha viongozi wa KDFA wanatuhumiwa kwa ubadhilifu wa Tshs
200,000,fulana na mipira 10 iliyotolewa na wadhamini wa michuano hiyo kampuni
ya vinywaji baridi ya Coca Cola kupitia shirikisho la soka TFF na vyama vya
soka vya mikoa.
"Ninachoweza kusema ni kwamba soka letu halitapiga
hatua ikiwa tutaendelea kuwakumbatia viongozi wababaishaji wenye roho ya
kinyama wasiostahili kusamehewa hata kidogo,wameshindwa kusikiliza kilio cha
watanzania,hawana mipango ya maendeleo,ni watu wanaokula hata kidogo cha
vijana,hawafai",alisema kiongozi mmoja Kilosa United aliyekataa kuandikwa
jina.
"Nafikri imefika wakati TFF na coca cola kuweka wazi
faida ya udhamini huu kwetu,kwani tunachoshuhudia kwa sasa ni kugeuzwa mabango
ya kutangaza biashara ya kampuni na wanaonufaika watu wachache wasiovuja jasho
wala kujua gharama za kuandaa timu.
"Ubabaishaji unaofanywa na KDFA
umetusikitisha,wanapaswa kubadilika,ikishindikana tutagomea michuano hiyo
mwakani,kwani tumechoka kuingia gharama za kuandaa timu,kulipa ada ya michuano
halafu mwisho wa siku timu inashindwa kusafirishwa,vipaji vya hawa vijana
vitaonekana wapi",alisema Ramadhani Mkomwa(Paparazi) kiongozi wa Rudewa
Stars
Ramadhani Mtakwisha mwakilishi wa vilabu katika chama cha
soka wilayani humo alikiri KDFA kushindwa kuisafirisha timu ya cop coca cola
kwa madai ya ukosefu wa fedha,huku akidai kuwa tatizo hilo limezikumba karibu
wilaya zote za mkoa wa Morogoro ambapo baadhi ya timu zilicheza mechi moja na
kurejea makwao
Katika michuano ya mwaka huu timu tano za Kilosa United
A,Behewa Stars,Kilosa United B,Tindiga FC na Kilosa Youth Kids zilishiriki
mashindano hayo na timu ya Kilosa United B ilifanikiwa kunyakua ubingwa lakini
haikuambulia zawadi yoyote
0 comments:
Post a Comment