Kiggi Makasy- nyota wa mchezo Simba v Express leo |
KIUNGO mpya wa Simba SC, Kiggi Makassy leo ameifungia bao lake
kwanza klabu hiyo, tangu ajiunge nayo mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Yanga. Kiggi,
aliifungia Simba bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 20 katika mechi ya
kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uganda, Express ‘Tai Mwekundu’ kwenye Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga.
Hata hivyo, bao hilo la Kiggi lilidumu kwa dakika 20 tu,
kwani dakika ya 40, Joseph Kaira aliwasawazishia Tai Wekundu na hadi kipyenga
cha mwisho, timu hizo zilitoka 1-1.
Jana mabingwa hao wa Ligi Kuu waliiichapa Toto African ya
Mwanza mabao 2-0 katika mechi kali ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa CCM
Kirumba mjini Mwanza.
Wakati huo huo: Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan
Cirkovic anatarajiwa kutua saa 8:45 usiku kutoka nyumbani kwao, Serbia
alikokuwa kwa mapumziko. Milo atatua na na dege la shirika la ndege la Uturuki.
0 comments:
Post a Comment