Monday, June 04, 2012

    KIBAO KIPYA CHA TWANGA PEPETA

    Wanamuziki wa Twanga Pepeta wakitumbuiza wimbo huo kwa waandishi wa Habari, ukumbi wa Mango Garden, kinondoni, Dar es Salaam mchana wa leo.

    Shamba la Twanga Lyrics
    Songwriter:      Greyson Semsekwa
    Release date:   1st May 2012
    Record Label: ASET (TWANGA PEPETA)

    CHORUS: (Twanga)
    Mbegu ndiyo chanzo cha mti mzuri utoao matunda,
    Tunda linanunuliwa linaliwa msimu unapita,
    Mti uko pale pale na unatoa mengine,                                                                          usiuchezee eeeeh! usilichezee Pepeta,
    baadhi ya watu potofu, wanapenda kuchoma moto maeneo sehemu isiyohusika
    Wanataka tuishi jangwani, wadau muwe makini
    Hawa watu gani, wana nia gani, watatuweka sehemu gani
    Hata baba mungu alipoumba dunia, hakusahau kuweka ile bustani ya Eden,
    Patric Kessy kilimo kwanza kagharamikia shamba lake na Fredito Mopao,
    Papa Musofe unakuja kuvuna Yusuphed, mohamed kilua, Amos Makalla, Side mdoe
    ni nani kakupa idhini ya kuvuna shamba langu eeeeee
    Nteze wa Nteze kibali kakupa nani
    Daudi Bwelela sehemu isiyohusika wanataka tuishi jangwani


    VOCAL: (Kupaza)
    Nilishasema nasisitiza kaza buti mama, kuadi fisadi anazidi kutumwa lengo kutuchanganya mama, ogopa sana anaye cheza na akili yako mama,
    ogopa sana anaye kunyanganya  ulichonacho mmmmh,
    oooh mama mama mama mti wetu wanaupopoa,
    naimani tukiwa makini tutafika mbali mama ee e e e uuu


    VOCAL: (Venus)
    Malisho ya wadudu na ndege wa angani, hutegemea mti wenye matunda wale
    Asha Baraka tia mbolea palilia mti umeeee,
    Walee wenye mpango mti udumae usikue usimee, washindwe na walegeeee hee hee hee, ima bureau, Abdul Tall, Dito Mopao, Daladala camp,
    wakutengwa, Garage Mchangani wakataze wasichomeeee
    wataniua njaa Steve jimmy wazee wa muarubaini bravo ooh!


    VOCAL: (Dogo rama)
    Roho mbaya haifai wamefanya kila mbinu kuteketeza shamba langu ma
    ili mti ufee matunda yasipatikane ng’o, ila wapenda fruit hawawezi kukubali mti uteketee huku wakionaona mti nyong’onyee mpaka kwenye shina lake, ono no no no Ismail sota mkude pesa.


    VOCAL: (Haji Ramadhani)
    Hila zenu hazijengiiii, zinaongeza chuki majungu fitina vinyongo vyenu
    havina sababu kwetu, Petie Man waulize tumewaudhi nini mbona mwatusakama tumewakosea nini, mbona mwataka vya wenzenu tengenezeni vyenu,
    au ujuzi mdogo, msione vyaelea jua vimeundwaaaah!


    VOCAL: (Luiser)
    Ni juhudi zangu

    ALL:
    Zangu

    VOCAL: (Luiser)
    Oooh..Oooh ni juhudi zangu eeh, wanaona wivu shamba langu latoa matunda kila mwaka, mimi ni mkulima stadi naalima kwenye udongo wenye rutuba.
    Karim Sospeter, Pascal, Mathew Kiongozi, George Mweisiga, Chiddy Kateta, Deo Muta aaah palilia shamba shamba langu eeeeh!
    Uuuuuuuuh shamba langu.


    VOCAL: (Mumin)
    Ukiona chapendeza jua kimegharamiwa, haraka haraka haina baraka nawahurumiwa wenye haraka ya mafanikio wanaotaka kuvuna bila ya kulima Baraka Msiilwa na Asha Baraka wametoka mbali wamefanya kazi kubwa kuliandaa kulilima na kulitunza shamba hili
    Na ndiyo maana mpaka leo shamba linahimili vishindo


    Shamba la Twanga Pepeta, Shamba la Twanga. Kisima cha burudani Shamba la Twanga Pepeta, Miaka mia moja
    Shamba la Twanga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIBAO KIPYA CHA TWANGA PEPETA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry