|
Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Vodacom Kevin Twisa 'Kifaa' |
|
Katikati ni Sumaye, kulia Twisa na kuhsoto Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) na mmiliki wa kituo cha Redio cha Voice Of Tabora |
|
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura kulia |
|
Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala kushoto na rafiki zake |
|
Twisa akihutubia |
|
Mwenyekiki wa Simba, Rage kulia, Mwenyekiti wa Azam, Mzee Mohamed Said katikati na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa |
|
Waziri Mkuu wa zamani, kipenzi cha Watanzania, Sumaye |
|
Msaidizi wa Sumaye, Chombo kulia akizungumza na bosi wake |
|
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kulia, katikati Twisa wakiwa na Sumaye |
|
Wadau, Dina Ismail kushoto na Mohamed Mharizo |
|
Warembo wa Vodacom |
|
Maswahiba wa miaka nenda, rudi, Grace Hoka, Mhariri wa BINGWA na Dina Ismail, wa dinaismail.blogspot.com ambaye pia ni Mwandashi wa Habari za Michezo Mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima |
|
Twisa kulia na Sumaye |
|
Rage na Sumaye wakiteta |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
BIN ZUBEIRY |
|
Mzee Said kulia, Mwesigwa na Jaffar Iddi, Msemaji wa Azam |
|
Vimwana wa Vodacom na mataji, tuzo mbalimbali walizokabidhiwa washindi |
|
Refa bora, Martine Sanya kulia akipokea tuzo yake kutoka kwa Mh Sumaye. Kushoto ni Twisa |
|
Rage amkimpokelea tuzo Kaseja |
|
Mzee Said akipokea tuzo |
|
Mwesigwa akipokea hundi ya Yanga |
|
Mzee Said akipokea tuzo ya Azam FC |
|
Rage akipokea hundi ya Simba SC |
|
Angetile akipongezana na Mh Sumaye |
|
Wadau wa Yanga, katika picha ya pamoja na Mh Sumaye |
|
Wadau wa Simba SC katika picha ya pamoja na Mh Sumaye |
|
Angetile kulia na kushoto Wambura katika picha ya pamoja na Sumaye |
|
Frank damayo |
|
Mlimbwende |
|
Damayo akipokea tuzo yake |
|
Damayo akichukua msosi |
|
Mh Mbunge na kiungo wa zamani wa Simba SC, Rage 'akifakamia' |
Na Prince Akbar
JUMA Kaseja, kipa wa Simba SC usiku huu ameibuka kipa bora
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 3.3
kutoka kwa wadhamini Vodacom.
Katika hafla ya kukabidhi tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
zilizofanyika kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton, Masaki, Dar es Salaam,
beki wa Azam FC, Aggrey Morris alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi
Kuu.
Aidha, Azam FC washindi wa pili wa Ligi Kuu walitwaa pia
tuzo za timu yenye nidhamu, wakati kocha waom, Stewart Hall kutoka Uingereza,
aliibuka kocha bora, mshambuliaji wake John Bocco ‘Adebayor’ aliibuka mfungaji
bora.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile
Osiah pia alitambulisha tuzo maalum kwa wachezaji chipukizi waliopandishwa
kutoka timu za vijana na kufanya vizuri katika timu za wakubwa.
Katika tuzo hizo, kiungo mpya wa Yanga, Frank Damayo
sambamba na Rashid Mandawa wa Coastal Union na Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting,
kila mmoja alitwaa Sh. Milioni 1.
Katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa
zamani, Frederick Sumaye, mwamuzi Martin Sanya alishinda tuzo ya refa bora,
wakati bingwa Simba alizawadiwa Milioni 50, mshindi wa pili Azam Milioni 22 na
Yanga aliyekuwa wa tatu Milioni 15.5.
0 comments:
Post a Comment