MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema
kwamba wataishitaki Yanga kwa kitendo cha kuzungumza na beki wao, Kelvin Patrick
Yondan kinyume cha kanuni za usajili.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY dakika chache zilizopita,
Kaburu (pichani kushoto) alisema kwamba kanuni za usajili haziruhusu klabu kuzungumza na mchezaji
wa klabu nyingine bila kupewa ruhusa na klabu yake.
“Kwa mujibu wa fomu tuliyoiona ambayo Yondan amesaini Yanga,
wakati anasaini Yanga alikuwa ana mkataba wa miezi sita na Simba, kisheria ni
makosa na sisi tutawashitaki kwa kukiuka kanuni za usajili,”alisema.
Inadaiwa Yondan alisaini Yanga, Novemba mwaka jana- wakati
ambao wenyewe (Yanga) wanadai alikuwa hana mkataba na Simba SC.
Yondan mwenyewe amekwishakaririwa akikana
kusaini Yanga, ingawa fomu ya mkataba imemuumbua leo. Mapema mwezi uliopita
Simba ilisema ilikwishongeza mkataba na Yondan.
0 comments:
Post a Comment