Wachezaji wa Azam |
Na Prince Akbar
JESHI limetimia Chamazi. Wachezaji wote waliosajiliwa na Azam
FC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na michuano ya
Afrika, leo asubuhi wamefanya mazoezi, kasoro tu Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
pekee, ambaye ni majeruhi.
Wachezaji waliokamilisha idadi ya kikosi kizima cha Wana
Lamba Lamba ni kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’,
ambao walikuwa wana udhuru.
Sasa, maandalizi ya Azam FC kwa ajioi klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame ni kama yameanza rasmi, huku Makocha Waingereza,
Stewart Hall na Msaidizi wake, Kalimangonga Sam Daniel Ongala wakiwa wenye
matumaini makubwa na kikosi chao.
Sure Boy Jr. aliyeumia mazoezi timu ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars ikiwa inajiandaa na mechi dhidi ya Msumbiji wiki mbili zilizopita, anaendelea
na programu maalum ya daktari wa timu hiyo na tayari ameripoti.
Azam, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
walikwishamalisha usajili wa wachezaji wao hata kabla ya kwenda likizo.
Programu ya maandalizi ya Kombe la Kagame, inayoendelea hivi
sasa itamalizika siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo, Juni 28 na
yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza
maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Maandalizi kwa ajili ya VPL yatahusisha pia ziara ya nje ya
nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema nchi hiyo itatajwa baadaye.
Wachezaji wapya kikosini Azam msimu huu ni kiungo Mkenya
George ‘Blackberry’ Odhiambo na kipa Deogratius Munishi kutoka Mtibwa Sugar,
wakati Aishi Salum, Jackson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph
Kimwaga, wamepandishwa kutoka akademi ya Azam.
Kikosi kamili cha Azam FC kinaundwa; na makipa, Mwadini
Ally, Deo Munishi ‘Dida’ Aishi Salum na Jackson Wandwi, mabeki wa Ibrahim
Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samir Haji Nuhu, Luckson Kakolaki, Said
Mourad, Joseph Owino na Aggrey Morris.
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum
Abubakar, Abdi Kassim Sadalla, Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam,
Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche,
Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati
washambuliaji ni Gaudence Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’.
Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza Kombe la Kagame, baada
ya kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu. Katika Kombe la
Kagame mwaka huu, wenyeji Bara wataingiza timu tatu, Yanga ambao ni mabingwa
watetezi, wakati Simba na Azam wanaingia kwa nafasi za uwakilishi.
Michuano ya Kagame
inatarajiwa kuanza Julai 14 hadi 29, mwaka huu na kuna uwezekano Azam FC
wakachezea mechi zao kwenye Uwanja wao wa Chamazi, kuwa michuano hiyo itafanyika
katika kituo kimoja tu, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment