NUSU Fainali zimejulikana baada ya mechi za Robo Fainali na kuna wachezaji ambao walionyesha viwango baab kubwa, kiasi cha kuzibeba timu zao katika hatua hiyo.
Langoni, Gianluigi Buffon aliokoa penalti ya Ashley Cole katika mikwaju mitano mitano usiku wa jana.
Langoni, Gianluigi Buffon aliokoa penalti ya Ashley Cole katika mikwaju mitano mitano usiku wa jana.
Katika beki, Glen Johnson alifanya vema katika mechi na Azzurri, wakati Pepe alisimama imara kwenye safu ya ulinzi ya Ureno, na hakuwaruhusu Czech kupiga mashuti ya kulenga lango. Mats Hummels alikuwa kizingiti katika ushindi wa Ujerumani wa 4-2 dhidi ya Ugiriki, wakati Jordi Alba alifanya vitu adimu katika kuzuia na kushambulia wakati Hispania ikiifunika Ufaransa.
Xabi Alonso alicheza mechi yake ya 100 huku akichangia kwa kiasi kikubwa La Roja kutinga Nusu Fainali. Andrea Pirlo amedhihirisha kuwa 'mapigo ya moyo' wa Italia kwa mara nyingine, akiumiliki vema mchezo dhidi ya England, kisha akafunga mkwaju wake wa penalti. Mtu mwingine aliyecheza soka baab kubwa kwa Ujerumani ni Sami Khedira, ambaye aling'ara dhidi ya Ugiriki.
Marco Reus na Miroslav Klose nao walikuwa hatari, wote walifunga mabao mazuri katika ushindi wa Ujerumani. Miwsho, Cristiano Ronaldo alikuwa shujaa wa Ureno kwa mara nyingine, akiipeleka timu yake Nusu Fainali kwa mabao ya kichwa. BIN ZUBEIRY kwa msaada wa Goal.com inakupa sasa wachezaji 11 wa kuunda kikosi bora cha Robo Fainali za Euro 2012.
BUFFON |
ITALIA |
JOHNSON | PEPE | HUMMELS | JORDI ALBA |
ENGLAND | URENO | UJERUMANI | HISPANIA |
XABI ALONSO | PIRLO | KHEDIRA |
HISPANIA | ITALIA | UJERUMANI |
REUS | KLOSE | RONALDO |
UJERUMANI | UJERUMANI | URENO |
0 comments:
Post a Comment