Diamond atapagawisha Miss Dar Inter College |
Na Princess Asia
MFALME wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa
kupamba shindano la kumsaka Miss Dar Inter College 2012, linalotarajiwa
kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, uliopo mkabala na chuo
cha Usimamizi wa Fedha, (IFM).
Mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail Mkinginye ‘Dodo’, ameiambia
BIN
ZUBEIRY leo kwamba mbali na Diamond, onyesho hilo pia litapambwa na
burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project
Fame, mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo
warembo 14 watakaosghiriki wanaendelea
na mazoezi katika hoteli ya The Grand
Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo
kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania
,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji
linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana,
Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina, ambaye ni mmiliki wa blog ya dinaismail.blogspot.com,
aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy
Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda,
Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo,
Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo wa gazeti la
Tanzania Daima, alisema shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kupitia bia ya Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada
Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions,
Grand Villa Hotel, Clouds Media Group na blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY,
Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
Baadhi ya washiriki Miss Dar Inter College mazoezini |
0 comments:
Post a Comment