// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DEIDRE LORENZ AWAPA 'LOVE' YATIMA MOSHI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DEIDRE LORENZ AWAPA 'LOVE' YATIMA MOSHI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 22, 2012

    DEIDRE LORENZ AWAPA 'LOVE' YATIMA MOSHI


    Lorenz akiwa Ngowi kushoto

    Na Princess Asia
    MCHEZA sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ambaye alitua mjini Moshi jana kushiriki kwenye mbio za kimataifa za Mt. Kilimanjaro Marathon leo alikaa na watoto wa kituo cha yatima cha Upendo kinachoendeshwa na masista wa shirika la Precious Blood mjini Moshi.
    Ofisa Uhusiano wa Mount Kilimanjaro Marathon, Grace Soka ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba, Lorenz aliingia kwa kishindo katika Manispaa ya Moshi na kueleza juu ya nia yake ya kuitangaza Tanzania nchini Marekni kwa kutumia usanii wake wa filamu.
    Amesema Deidre Lorenz anashiriki katika mashindano ya Mt. Kilimanjaro Marathon ambayo yanaanza kutimua vumbi tarehe 24 Jumapili kuanzia Moshi klabu hadi Rau madukani na kurudi.
    Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na Marie Frances kutoka katika mji wa Bethesda nchini Marekni mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
    Amesema Deidre Lorenz anawakilisha kikundi cha Actors Guild ambacho kina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa saratani. Katika ziara yake kwenye kituo cha watoto yatima cha Upendo Deidre aliwasomea watoto hao hadithi mbalimbali za watoto.
    Aidha, aliwapa zawadi za fangi za kuchora, vitabu, daftari, kalamu, chocolate na zawadi nyingine kemkem zinazowaelimisha watoto.
    Amesema Lorenz ameshiriki pia katika mahojiano na waandishi mbalimbali wa habari mjini Moshi na kueleza kuhusu nia yake ya kuitembelea Tanzania mara kwa mara. Amesema kuwa wazazi wake hususan bibi yake alimwambia kuwa Tanzania ni nchi yenye wanawake wenye sura nzuri sana. Aidha marafiki zake wamemwambia kuwa aje yeye kwanza ili wao waje katika mbio zinazofuata.
    Amesema klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 inakusudia kuwatumia watu maarufu kuja Tanzania ili waweze kuutangaza utalii pamoja na mazingira ya kuwekeza. Klabu hii ina lengo la kuanzisha marathon nyingine tena ambayo itajumuisha mbio na michezo mingine ya uwanjani.
    “Tutakuwa na wiki nzima ya mashindanio ya uwanjani na siku ya saba tutafanya mbio za marathon” alisema Rais wa Klabu hiyo Onesmo Ngowi alipokuwa anazungumza na waandishi wa bahari hapa Moshi. Ngowi alieleza kuwa ni muhimu Moshi/Tanzania ikawa na mashindano ya michezo mingi itakayowavutia watalii na wawekezaji wengi kuja Tanzania,”amesema.
    Akielezea kuhusu mikakati ya klabu yake kuendeleza mchezo wa riadha Ngowi ambaye pia ni Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi alisema kuwa wameweka mikakati mingi itakayoifanya mji wa Moshi kuwa kitovu cha utalii katika mkoa wa Kilimanjaro.
    Hizi mbio ni sehemu tu ya mikakati ya kuendeleza michezo katika mkoa huu ambao miaka ya sabini ulikuwa unaongoza kwa michezo katika nchi hii. “Tutashirikiana na mashirikisho ya michezo ya ndani na nje kuinua viwango vya wanamichezo wetu” alisema Ngowi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo katika mkoa wa Kilimanjaro. Alisema kuwa wameandaa mikakati mingi na kumalizia kuwa Tanzania ni yetu sote kwa hiyo tuna jukumu la kuchangia katika maendeleo yake.
    Deidre Lorenz atakimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili ijayo na ataondoka usiku wa jumapili kurudi nyumbani kwake New York jiji linajulikana kama “The Big Apple” na Financial Capital of the World (Jiji la Fedha Duniani)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEIDRE LORENZ AWAPA 'LOVE' YATIMA MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top