// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CLUB E KUFANYA SHOO LA KI HOLLYWOOD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CLUB E KUFANYA SHOO LA KI HOLLYWOOD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 19, 2012

    CLUB E KUFANYA SHOO LA KI HOLLYWOOD


    Wenge ya werason
    Na Princess Asia
    KWA mara nyingine tena, Embassy kupitia chapa yake ya Club E inakuja na pati ya aina yake inayojulikana kama Hollywood Glam night. Ni Pati ya kipekee itakayoleta mandhari ya Hollywood jijini Dar es salaam. Pati hii ya aina yake itafanyika ijumaa hii tarehe 22 katika ukumbi wa Blue Pearl ulioko Ubungo Plaza kuanzia saa mbili usiku.
    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Paul Makanza, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Sigara (TCC), pati hii yenye maudhui ya Hollywood itakuwa ya kwanza jijini Dar Es Salaam ambapo wanachama na wapenzi wa burudani watapata wasaa wa kuona burudani mbalimbali na vivutio vya mandhari ya Hollywood ambazo zimeandaliwa mahsusi kwa ajili ya wanachama wa Club E.
    Wanachama wa Club E wataingia bure kwenye pati hii kwa kupitia mwaliko maalum na kwa watu wengine ambao si wanachama wa Club E na wangependa kuhudhuria kwenye pati hii, watalipa shillingi 30,000 tu za kitanzania. Kiingilio hiki kitajumuisha vinywaji pamoja na chakula.
    Kwa miaka mitano iliyopita, Club E imejijengea jina kwa kufanya pati zenye ubora na hadhi ya hali ya juu kwa wanachama wake. Ukiacha swala la kuburudisha wanachama wake, Kwa kipindi cha miaka mitano Club E pia imeweza kutoa mchango wake kwa kuinua wanamuziki wetu wa ndani ambao wamepata wasaa wa kuimba kwenye jukwaa moja na wasanii mbalimbali wa bara la Afrika na Marekani. 
    Club E ilianzishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwaleta pamoja na kuwaburudisha wanachama wake ambao ni wavutaji wa sigara ya Embassy. Tangia kuanzishwa kwake Club E imefanya pati nyingi na kuwaleta wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi kutumbuiza. Wasanii walioletwa Club E ni pamoja na Werrason, Miriam Makeba, Amani , Blue 3, Lady Jay Dee, Mbilia Bell, Tshalla Muana, JB Mpiana, Fm academia, Chaka Khan na Falii Ipupa.
    Wanachamawa Club E wategemee pati ya aina yake ijumaa hii na tunahimiza wasikose kuja kushuhudia pati hii itakayokuwa ya kipekee itakayosheheni burudani mbalimbali. Kwa ambao si wanachama wa Club E tiketi zinapatikana Steers mjini, Engen Petrol Station Mbezi, Mile PambaMwenge, Club MaishaOysterbay, Steers Kijitonyamana TCC Club Chang’ombe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CLUB E KUFANYA SHOO LA KI HOLLYWOOD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top