Tetesi za Alhamisi magazeti ya Ulaya


CHELSEA MBIO KUNASA BONGE LA KIFAA DUNIA NZIMA HAKUNA

KLABU ya Chelsea, ipo karibu kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic, mwenye umri wa miaka 22, baada ya kuambiwa wanaweza kmumpata kwa dau la pauni Milioni 25.
Former Manchester United striker Michael Owen
Al-Shabab yamkana Michael Owen
KLABU ya Napoli imeziambia Manchester City na Chelsea zisahau kumsajili mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uruguay, Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU ya Al-Shabab ya Falme za Kiarabu (UAE) imesema haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen baada ya kutemwa na klabu yake, Manchester Unite. Habari kamili: Daily Mirror 
KLABU ya Tottenham inaweza kuonja machungu ya kumpoteza Luka Modric aliye mbioni kutimkia Real Madrid na imejiandaa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uturuki, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23, azibe pengo lake.
BEKI wa Ajax, Jan Vertonghen anatumai kutimkia Tottenham Hotspur kwa dau la pauni Milioni 9.5 umefifia kutokana na mkataba wake wa makato ya asilimia 15 ya mauzo yake.
NYOTA wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek anaongoza katika orodha ya kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo ya mabeki wapya wa kulia wanaotakiwa na klabu hiyo.
Kuban Krasnodar striker Lacina Traore
Lacina Troare anatakiwa na Liverpool
KLABU ya Liverpool iko tayari kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Lacina Traore, mwenye umri wa miaka 22, kutoka Kuban Krasnodar ya Urusi.
KLABU ya Sunderland inataka kuwaachia Ahmed Elmohamady na George McCartney waende West Ham mwishoni mwa mwezi huu.

EURO 2012

WAPIKA sheria za soka watathibitisha sheria ya teknolojia katika mstari wa lango wiki ijayo, baada ya marefa kushindwa kuwapa bao Ukraine dhidi ya England.
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ametimkia Los Angeles kwa mapumziko mafupi baada ya timu yake ya taifa, England kutolewa katika Euro 2012.

WACHEZAJI WOTE WAKIMBIA

KLABU ya Rangers itaanza maandalizi ya msimu mpya na wachezaji watatu tu, kutokana na wachezaji wengine kugoma kwa sababu ya mishahara midogo na wameamua kuondoka.
Lokomotiv Moscow and Croatia defender Vedran Corluka
Vedran Corluka amejiunga na Lokomotiv Moscow
NAYE Roman Pavlyuchenko amewaambia Lokomotiv Moscow wamepata beki bora kutoka Tottenham, kwa kumsajili Vedran Corluka. Habari kamili: Daily Mail 
MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Olivier Giroud ndiye mtu anayetarajiwa kumaliza ukame wa mataji wa miaka saba kwa Washika Bunduki hao wa London, amesema kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Stewart Robson.

BIRMINGHAM SURA NYEKUNDU...

KLABU ya Birmingham City imekasirishwa na kitendo cha habari za kumteua Lee Clark kuwa kocha wao mpya, kuvujishwa kwenye internet - na mtoto wake.