Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya
MAN UNITED, MAN CITY ZAISHIA KUNAWA KWA NYOTA WA BUNDESLIGA
MCHEZAJI anayewaniwa na klabu za Man United na Man City, Mats Hummels, mwenye umri wa miaka 23, ameamua kubaki Borussia Dortmund baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano.
NYOTA wa Spurs, Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 22, amekwenda mapumzikoni kufikiria mustakabali wake katika klabu ya Tottenham huku tetesi zikisema hatima yake itategemea na mustakabali wa kocha Harry Redknapp klabuni.
KLABU za QPR, West Brom na Malaga zote zinammezea mate kipa wa West Ham, Robert Green, mwenye umri wa miaka 32, baada ya Mwenyekiti wa Hammers, David Gold kuthibitisha kwamba kipa huyo wa England anaweza kuondoka.
KIUNGO wa Tottenham, Steven Pienaar, mwenye umri wa miaka 30, anahofia Spurs itamuuza kurejea Everton, ambako alicheza kwa mkopo mwishoni mwa msimu.
MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester City wanataka kumsajili nahodha wa Newcastle United, Fabricio Coloccini, mwenye umri wa miaka 30 .
KLABU ya West Ham imeambiwa ilipe pauni Milioni 6 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa Norwich, Grant Holt, 31.
KLABU ya Chelsea inataka kuifuata saini ya Eden Hazard na Marko Marin na kujaribu kuwang'oa Arsenal, wachezaji wawili Bacary Sagna, mwenye umri wa miaka 29 na Theo Walcott, mwenye miaka 23.
NORWICH ITABAKI LIGI KUU
BEKI wa Norwich, Russell Martin, mwenye umri wa miaka 26, anaamini kocha mpya ataendelea kuifanya timu hiyo ibaki Ligi Kuu England kwa msimu wa pili.
MESSI AMJAZA MIMBA BINTI WA WATU
NYOTA wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi tetesi zimezagaa kwamba mpenzi wake ni mja mzito wakitarajia kupata mtoto wa kwanza na hilo alilidhihirisha katika ushangiliaji wa bao lake dhidi ya Ecuador. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliweka mpira mpele ya jezi yake na 'kuonyesha ishara ya mimba' akishangilia na mashabiki.
0 comments:
Post a Comment