KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Salum Machaku (pichani kulia) anaweza kutolewa
kwa mkopo kwa nusu msimu, ili ajifundishe adabu- kwani hivi sasa mabega
yamepanda mno juu.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani
ya Simba, zimesema kwamba Machaku amekuwa akijisikia mno baada ya kufanya
vizuri kidogo msimu huu akiwa na jezi ya Wekundu wa Msimbazi, kiasi kwamba
amekuwa akidharau hadi viongozi.
Kiongozi mmoja wa juu wa Simba, aliiambia BIN
ZUBEIRY wiki hii kwamba uongozi ulifanya jitihada kubwa za kumbadili
kitabia Machaku, ikiwemo kumuweka chini ya mchezaji anayeogopwa na wachezaji
wote, Haruna Moshi ‘Boban’, lakini ikashindikana.
“Sasa tunataka tumpe nafasi ya mwisho, tumpeleke kwa mkopo
klabu nyingine akacheze mzunguko mmoja
tu, akijirekebisha, tunamrudisha, ikishindikana ndio imetoka,”alisema kiongozi
huyo.
Wakati huo huo, Machaku ni kati ya wachezaji ambao wamo
kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na mahasimu wa jadi wa Simba, Yanga. Na katika
siku za karibuni, Machaku amekuwa karibu mno na kipa wa Yanga, Shaaban Hassan Kado
ambaye waliwahi kucheza naye pamoja Mtibwa Sugar na timu ya taifa.
0 comments:
Post a Comment