Na Prince Akbar
MSHAMBULIAJI wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis
Mrwanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Simba, ambao hauna
kipengele cha kumruhusu kuuvunja kabla haujamalizika.
Mrwanda (pichani kushoto), awali ilielezwa anataka kusaini mkataba ambao
wakati wowote akipata timu nje, aondoke, lakini kwa mujibu wa mkataba aliosaini
Simba ni kwamba akipata timu italazimika kumnunua kutoka kwa Wekundu wa
Msimbazi, au isubiri hadi amalize mkataba.
Habari za uhakika, kutoka ndani ya Simba SC ambazo BIN
ZUBEIRY imezipata, zimesema kwamba Mrwanda ameridhika na mkataba huo na
ameahidi kufanya vitu baab kubwa Msimbazi.
Kwa upande mwingine, Simba SC imeamua kumtema kiungo Salum
Machaku kwa makubaliano maalum ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba. Simba
ilitaka kumtoa kwa mkopo Machaku, lakini mwenyewe akasema bora aachwe moja kwa
moja.
Tayari Simba
imemsajili kiungo wa Yanga, Kiggi Makassy kuziba nafasi ya Machaku. Machaku sasa
ameingia kwenye mazungumzo na Yanga.
0 comments:
Post a Comment