BEKI wa kulia wa Simba SC, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kipa
William Mweta huenda wakatemwa na klabu hiyo, kutokana na ripoti ya daktari wa klabu
hiyo, Cossmas Kapinga kusema kwamba wawili hao ni wajeruhi wa muda mrefu.
“Ripoti niliyoiwasilisha kwa uongozi nimesema wazi kuhusu
wachezaji hao, kwamba ni majeruhi wa muda mrefu, wanaweza kuwa nje miezi zaidi
ya mitatu,”alisema Kapinga alipozungumza na BIN ZUBEIRY mchana huu.
Katika kutafuta mustakabali wa wachezaji hao, BIN
ZUBEIRY ilizungumza na Mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Simba,
ambaye alisema kwamba uongozi utakutana wakati wowote kuamua hatima ya
wachezaji hao na zaidi wanaweza kuondolewa kwenye usajili.
“Hawataachwa moja kwa moja, wataendelea kuhudumiwa na klabu,
kila kitu kulingana na mikataba yao, ila wataondolewa kwenye usajili, kwa
sababu watakuwa wanajaza nafasi wakati hawawezi kucheza.
Klabu itawahudumia
vizuri, wakipona kama mzunguko wa pili au hata msimu ujao, watarudishwa
kikosini,”alisema Mjumbe huyo.
0 comments:
Post a Comment