MSHAMBULIAJI mtata wa Italia na Manchester City, Mario Balotelli alimkasirikia mwandishi wa habari aliyekuwa anafuatilia nyendo zake nje hya kambi ya timu mjini Krakow.
Nyota huyo wa zamani wa Inter Milan, alitemwa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Jamhuri ya Republic Jumatatu, lakini akatokea benchi na kuingia uwanjani na kwenda kufunga bao la pili, kikosi cha Cesare Prandelli kikishinda 2-0. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, staili yake ya kushangilia bao hilo ilikuwa utata mtupu, pamoja na kuonekana akifoka kwenye benchi la Italia kumuelekezea maneno mchezaji mwenzake, Leonardo Bonucci afunge mdomo wake. Na mshambuliaji huyo ameripotiwa kuingia kwenye utata zaidi baada ya kuzozana na paparazzi wakati akitembea madukani karibu na kambi ya Italia, mjini Krakow, Poland. "Nakwenda kula ice cream katika jengo na kurudi hotelini kula chakula cha usiku. Unataka mimi nifanye nini?" Balotelli amekuwa maarufu kwenye vyombo vya habari katika Euro 2012 baada ya kukumbana na hila za kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa Croatia. Mechi ijayo ya The Azzurri ni Robo Fainali dhidi ya England mjini Kiev Jumapili.

0 comments:
Post a Comment