Wachezaji wa Azam A |
KLABU ya Azam FC imeshindwa kutamba mbele ya vijana wao Azam Academy kwa kukubali kufungwa 3-2, katika mchezo wa kujipima uliopigwa leo asubuhi kwenye uwanja wa Azam Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa marudiano ulichezwa kwa dhumuni la kujipim timu zote zikiwa kwenye maandalizi, Azam FC inajiandaa kushiriki Kombe la Kagame na mashindano ya Ujirani mwema, Azam Academy wao wanajiandaa kushiriki michuano ya vijana Rolling Stone itakayofanyika nchini Burundi.
Katika mchezo huo Azam FC walikuwa wa kwanza bao kupitia kwa Zahor Pazi aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko madabiliko ambayo yalikuwa na manufaa kwa Academy ambao katika dk ya 46 Joseph Kimwaga alisawazisha bao akicheza vyema krosi ya Ahmed Abas na kubadilisha matokeo kuwa 1-1.
Academy walicheza kwa kasi kuzidi Azam FC, dk 65 kosa la beki ya Academy iliwaptaia Azam FC bao la pili lililofungwa na mshambuliaji Gaudence Mwaikimba, matokeo yakawa Azam FC 2-1 Academy.
Academy hawakukata tamaa wakaoongeza mashambulizi na dk 72 Kelvin Friday aliisawazisha bao hilo shuti la mbali na kubadili matokeo kuwa 2-2.
Mpira uliendelea timu zote ziliongeza jitihada za kuhakikisha wanapata bao la ushindi, Academy walifanikiwa kufanya shambulio hatari dakika mbili kabla mpira kumalizika na kupata goli la ushindi lililofungwa na mshambuliaji Jamir Mchaulu alimalizia pasi ya Kelvin na kuandika bao lilowatoa Academy kifua mbele kwa ushindi wa 3-1.
Azam Academy Aishi Salum, Dizan Issa, Reina Mgungula/Ismail Adam,Mohamed Hussein, Kelvin Friday, Ally Kaijage/Braison Raphael, Joseph Kimwaga/Jamir Mchaulu, Farid Musa/Abdul Mgaya, Deogratias Names/Ally Aziz na Assad Ally/Ahmed Abbas.
Azam FC, Wandwi William, Ibrahim Shikanda/Said Morad, Joseph Owino/Himid Mao/Luckson Kakolaki, Luckson Kakolaki/HImd Mao, Ibrahim Mwaipopo/Ramadhan Chombo, George Odhiambo/Mwaikimba, Abdulghan Gulam/Abdulhalim Humud, Samir Haji Nuhu/Michael KIpre na Zahor Pazi/KIpre Tchetche.
0 comments:
Post a Comment