Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya


ARSENAL WAKUBALI KUMUUZA VAN PERSIE PAUNI MILIONI 30

HATIMAYE klabu ya Arsenal imekubali kumuuza mshambuliaji wake Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, kwa dau la pauni Milioni 30 - na winga wa Washika Bunduki hao, Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23, anaweza pia kumfuata Mholanzi huyo katika mlango wa kutokea.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amepanga kusajili wachezaji wawili wa Ufaransa, Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, na Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 21.
KOCHA Mreno, Jose Mourninho atajaribu kuinasa saini ya kiungo mchezeshaji wa kimataifa wa Hispania, David Silva, mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa anachezea klabu bingwa England, Manchester City ili ahamishie cheche zake Real Madrid.
Gylfi Sigurdsson
Gylfi Sigurdsson.
KLABU ya Manchester United inamuwania kiungo wa klabu ya Hoffenheim, Gylfi Sigurdsson, mwenye umri wa miaka 22, huku kocha Sir Alex Ferguson akitunisha misuli ili kuipiku Liverpool inayomuwania pia.
KLABU ya Manchester United inataka kutumia fursa ya kufukuzwa kazi kwa Harry Redknapp katika klabu ya Tottenham kwa kusajili wachezaji wawili wa klabu hiyo ya London, kiungo Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, na winga Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 22.
KLABU ya Tottenham inapambana kuipiga bao Newcastle katika mbio za kuwania saini ya winga wa Manchester United, kindaEzekiel Fryers, mwenye umri wa miaka 19, baada ya beki huyo kugoma kuendelea kuichezea klabu hiyo mkataba wake utakapoisha mwezi ujao.
MSHAMBULIAJI Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 22, anataka kuondoka Chelsea baada ya kukosa Euro 2012, huku Arsenal, Manchester City, Tottenham na Liverpool zote zikiwa tayari kumsajili.
KLABU ya QPR itakamilisha mpango wa kumsajili kipa wa West Ham, Robert Green wakati mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32-akiwa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.
KLABU ya West Ham ipo kwenye mazungumzo na Juventus kwa ajili ya winga Eljero Elia, mwenye umri wa miaka 25, na wanajadili pia uhamisho wa mshambuliaji Luc Castaignos, mwenye umri wa miaka 19, na Inter Milan.

TETESI ZA EURO 2012

MSHAMBULIAJI wa Hispania, Alvaro Negredo amesema kwamba mabingwa hao wa dunia na Ulaya ni bora wakutane kuliko Ufaransa katika Robo Fainali.
Christian Eriksen
Christian Eriksen aliripotiwa kutakiwa na Manchester United, Manchester City, Arsenal na Chelsea
GWIJI wa Denmark, Jan Molby amesema kwamba kiwango kibovu cha Christian Eriksen katika Euro 2012 kinadhihirisha mwanasoka huyo wa kimataifa wa Denmark hayuko tayari kuhamia klabu kubwa Ulaya.
BEKI wa Croatia, Vedran Corluka, mwenye umri wa miaka 26, bado anataka kuondoka Tottenham licha ya kuondoka kwa kocha Harry Redknapp.
AVB APEWA MIAKA MIWILI SPURS
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas ameripotiwa kupewa mkataba wa miaka mitatu na Tottenham akarithi mikoba ya Harry Redknapp.
Laurent Blanc
Laurent Blanc.
KOCHA wa Ufaransa, Laurent Blanc naye anatajwa kuwa mbioni kumpiga bao Villas-Boas katika kuwania kurithi mikoba ya Harry Redknapp kama kocha wa Spurs. Habari kamili: Sunday Mirror 
NDOTO za Tottenham kumnasa David Moyes zimeingia dalili za kuyeyuka baada ya kocha huyo kuwa katika mpango wa kusaini mkataba mpya na Everton.
KLABU ya Tottenham ilijiandaa kumtupia virago Harry Redknapp tangu miezi sita iliyopita.
MCHEZAJI anayewaniwa na Arsenal, Alan Dzagoev, mwenye umri wa miaka 21, mshambuliaji wa kimataifa wa Urusi, amesema kwamba yuko tayari kwa dili hilo la kumtoa CSKA Moscow ya nyumbani kwao.
KIUNGO wa Manchester United, Luis Nani, mwenye umri wa miaka 25, anahofia anaweza kulazimika kuondoka Manchester United kutokana na klabu hiyo kusuasua kumpa mkataba mpya.