Yaya |
KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure yu tayari kwa changamoto mpya msimu ujao, wakala wake amesema.
Nyota huyo wa Ivory Coast mustakabali wake katika Ligi Kuu ya England umekuwa shakani tangu asema wiki iliyopita kwamba anatamani kurejea Barcelona akamalizie soka yake huko baada ya kukipiga Camp Nou kati ya mwaka 2007 na 2010.
Kocha wa City, Roberto Mancini tangu wakati huo amepuuza madai kwamba Toure hafurahii katika klabu hiyo, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameendelea na mipango yake.
"Amefanya kila alichoweza City na anahitaji mvuto mpya," Dimitri Seluk alisema. "Toure angependa changamoto mpya. Haitamgharimu sana. Amebakiza miaka miwili katika klabu na mwaka mmoja anaweza kuondoka kwa mujibu wa sheria za Webster."
Seluk kisha amehakikisha hakuna mazungumzo yaliyofanyika na Barca, lakini amesema angependa kumrudisha mteja wake Camp Nou.
"Toure anaweza kusaini klabu yoyote kubwa, kama Chelsea na Bayern [Munich]," alisema. "Zaidi ya hapo anapenda kuona Barca inajiunga katika mbio za kuwania saini yake. Sijazungumza naye [kocha mpya wa Barca] Tito Vilanova au [rais] Sandro Rosell, lakini wanafahamu hali hiyo na kama wana nia na mchezaji huyo hakutakuwa na tatizo kuketi chini na kuzungumza."
Wakala huyo pia amefungua milango kwa mchezaji huyo kuhamia Real Madrid, akisema kwamba kocha Jose Mourinho ni shabiki mkubwa wa mteja wake.
"Sijui kama Madrid wana nia na Toure, Lakini nafahamu kwamba Mourinho amekuwa akimpenda sana tangu alipokuwa Chelsea," Seluk alisema. "Pia alimtaka alipohamia Inter, lakini Toure alikuwa Barca."

0 comments:
Post a Comment