• HABARI MPYA

        Wednesday, May 23, 2012

        WINGA WA LEOPARDS ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA


        Image

        Salim Kinje

        WINGA Salim Kinje ametangaza kuondoka AFC Leopards ya Kenya na kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, timu ya Simba ya Dar es Salaam.
        Habari zilizopatikana kutoka Nairobi na kukaririwa kwenye mtandao wa, SuperSport.com
        zimeeleza kuwa mchezaji huyo raia wa Tanzania, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuchezea timu hiyo.
        Kwa mujibu wa taarifa hizo, uamuzi huo wa Kinje kujiunga na Simba una nia ya kumuwezesha
        kuonesha kiwango chake ili aweze kuchezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ambayo ndiyo ndoto yake kubwa.
        Kocha Mkuu wa AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, Jan Koops amethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambaye pia humudu nafasi zote za kiungo na kusema kuwa hana muda mrefu watamkosa wakati wa kipindi cha usajili mwezi ujao.
        Alisema Kinje alimjulisha jana kwamba amepata dau zuri Simba na anaondoka na kwamba amewasisitiza anahitaji kurudi nyumbani kucheza soka.
        "Amenijulisha amepata ofa nzuri Simba na anaondoka, yeye ni Mtanzania anahitaji kurudi kwao kucheza soka.
        “Ni mchezaji mzuri, tunapoteza mtu muhimu, alikuwa zaidi ya mchezaji, alikuwa nahodha
        msaidizi na ndiyo utakapoelewa tumepoteza mchezaji wa aina gani," alisema kocha huyo.
        Kinje ambaye amepata kuchezea Sofapaka ya Kenya, kuna wakati aliripotiwa kutakiwa kuitwa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars', wakiamini alikuwa Mkenya, lakini
        uamuzi huo haukutekelezwa kutokana na yeye kuwa raia wa Tanzania na hakuwa tayari
        kuupoteza. 
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: WINGA WA LEOPARDS ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry