MSHAMBULIAJI Robin van Persie wa Arsenal, kesho anatarajiwa kuwa na kikao kizito na kocha wa klabu yake, Arsene Wenger na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis kuzungumzia mustakabli wake kwa Washika Bunduki hao.
Majadiliano hayo, yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Wenger, kuanzia saa 4:00 kwa saa za Uingereza.
Uamujzi wa mwisho utachukuliwa kabla ya kutajwa kwa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi Alhamisi, kinachotarajiwa kushiriki Euro 2012 na Van Persie anatarajiwa kuwamo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake, amemaliza msimu na mabao 41 katika mechi 53 za klabu na nchi yake.
Akiwa amefunga mabao 37 katika 48 za Arsenal na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa mabao yake 30 kwenye mechi 38, Van Persie sasa amegeuka lulu na klabu nyingi kubwa Ulaya zinataka kumsajili
0 comments:
Post a Comment