Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya
ABRAMOVICH AMNASA HAZARD, MANCHESTER UNITED WALIE TU
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kumnasa winga wa Lille, Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 21, baada ya kukubaliwa kumnunua kwa dau la pauni Milioni 32, kwa mkataba wa miaka mitano, utakaomfanya Mbelgiji huyo apate mshahara wa pauni Milioni 4.8 kwa msimu.
KLABU ya AC Milan inajaribu kupunguza bei ya mauzo ya kiungo wa Liverpool, mwenye umri wa miaka 27, Alberto Aquilani.
KLABU ya Barcelona inataka kumsajili beki mwenye umri wa miaka 28 wa Chelsea, Branislav Ivanovic.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameripotiwa kutenga dau kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Man City, Nigel De Jong, mwenye umri wa miaka 27, katika sehemu ya mpango wake kuimarisha kikosi chake msimu ujao.
MCHEZAJI anayewaniwa kwa muda mrefu na Arsenal, Mathieu Valbuena, mwenye umri wa miaka 27, hataondoka Marseille msimu huu, amethibitisha.
KLABU ya Newcastle United inataka kuendelea na mapinduzi ya Kifaransa kikosini mwao, sasa wakiwa mbioni kumsajili beki wa pembeni wa Lille, Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 26, baada ya kumuona aking'ara katika mechi dhidi ya Iceland mwishoni mwa wiki.
KLABU za Reading, Southampton na West Ham zote zinamtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Yakubu, mwenye umri wa miaka 29, ambaye anahama Blackburn iliyoshuka daraja.
NYOTA wa Ivory Coast, Salomon Kalou, mwenye umri wa miaka 26, anajiandaa kuachana na soka ya England na kusaini kwa mabingwa wa Ujerumani, Schalke baada ya mkataba wake wa sasa wa Chelsea kufikia tamati.
VAN GAAL KUTANGAZWA LIVERPOOL
Louis van Gaal anaamini Liverpool itataoa tamko rasmi juu ya kuteuliwa kwake mwishoni mwa wiki hii, licha ya kwamba mazungumzo kati ya Wekundu hao na kocha wa Wigan, Roberto Martinez bado yanaendelea.
WAMILIKI wa Liverpool watakuwa England leo kupiga hatua ya harakati zao za kusaka kocha mpya, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Wigan Athletic, Dave Whelan, watakuwa na saa 48 za kuamua kama Roberto Martínez ndiye atakuwa mrithi wa Kenny Dalglish aliyefukuzwa.
KLABU ya Tottenham Hotspur imemtambulisha kocha wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas kama mtu anayefaa kurithi mikoba ya kocha wao wa sasa, Harry Redknapp.
Laurent Blanc amesema kwamba kikosi cha Ufaransa hakiko tayari kuivaa England Juni 11 baada ya kulazimika kutoka nyuma kwa mabao 2-0 kuifunga Iceland.
John Fashanu amesema kwamba Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) halitilii mkazo ubaguzi na itamuwia vigumu kwenda kushuhudia England ikicheza na Ukraine.
HAZARD ALA BAGA
MCHEZAJI anayewindwa na Chelsea, Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 21, amekutwa anakula baga nje ya Uwanja wakati wa mechi ya Ubelgiji, ambayo yeye alitokea benchi ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment