// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAPI INAELEKEA LIGI KUU YETU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAPI INAELEKEA LIGI KUU YETU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 01, 2012

    WAPI INAELEKEA LIGI KUU YETU?


    Ni mdudu gani aliyeisibu ligi yetu! Send to a friend
    Monday, 30 April 2012 14:32
    NI dhahiri kwamba Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara maarufu Vodacom League inamalizika mwisho wa wiki.
    Nimeambiwa kwamba unaosubiriwa ni mchezo baina ya Simba na Yanga, hapo Mei 5 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hakuna shaka kwamba ligi ya mwaka huu imekuwa si yenye ushindani peke yake, bali kila aina ya vituko, visa na hata vimbwanga.
    Siwezi kuyarejea matukio yote ya ligi ya msimu huu kwani ni mengi sana.
    Lakini, kikubwa ni utovu wa nidhamu ambao umefanyika ndani na nje ya uwanja, kiasi cha kuathiri mwenendo na hata utamu wa ligi yetu.
    HATA kama klabu ya Simba itakuwa bingwa wa Tanzania Bara siku ya Jumamosi, huku ikiwaacha watani zake Yanga wakiwa watazamaji, kuna kitu kimoja cha kujiuliza.
    Ni dhahiri Yanga inasaka zaidi heshima Jumamosi ile kwa kutaka kufunga Simba, lakini lazima viongozi na mashabiki wa klabu hizi mbili wajiulize swali moja au zaidi.
    Swali la kwanza ni lile  linalohusu mustakabali wao kwenye michuano hii kwa miaka michache ijayo, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba klabu hizi hazivutii tena, hazina jipya katika soka ya kisasa.
    Ni klabu ambazo zinanolewa na makocha wa kigeni, zinao wachezaji kadhaa wa kigeni, lakini ndizo pia zimeshindwa kuibua na kuendeleza vipaji miongoni mwa vijana wetu wengi wa Kitanzania, ambao ni wapenda soka.
    Matokeo yake, mashabiki wengi wameendelea kuzishabikia klabu maarufu za Ulaya, Man United ambayo leo jioni inacheza na jirani yake, Man City kwenye Uwanja wa Etihad, kusaka nani atakuwa bingwa wa England msimu huu.
    Pia, tumewaona wengi wakikaa macho karibu usiku wote wakisubiri mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Barcelona na Chelsea au Real Madrid na Bayern Munich.
    Pili, unaweza kujiuliza, hivi mashabiki wetu wa Kitanzania wanaweza kukosa tu usingizi wao kwa nini? Kisa  au sababu ya klabu maarufu za Ulaya, kulikoni katika soka yetu?
    Majibu ni rahisi, kwamba klabu zetu, soka yetu haina lolote jipya na matokeo yake, mashabiki wanazishangilia klabu za nje, kuliko zetu, Yanga, Simba au kwa siku za karibvuni Azam FC.
    Ninaizungumzia Azam FC, kwanza nikilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lifanye uchunguzi wa kina na kuweza kubaini ni zipi sababu za ghasia na vurugu hizo kubwa kuwahi kutokea katika soka nchini, karibu zote zimehusisha klabu hiyo yenye umri wa miaka mitatu au zaidi kidogo?
    Binafsi, ninatambua kwamba wachezaji kadhaa wameadhibiwa, waamuzi wamesimamishwa, klabu zimetozwa faini, lakini sioni TFF wakifanya uchunguzi wa kubaini kulikoni, vurugu hizo zikahusisha klabu moja tu?
    Hii ni changamoto ambayo ninawaachia wao, yaani uongozi mzima wa TFF na kamati zake ili wachunguze, kisha watueleze  sababu za kisayansi za kwa nini hali kama hii?
    Inafaa watueleze ni nini kilichotokea katika mechi za ligi msimu huu na kwa nini zote zilihusisha klabu hii mpya na tajiri ambayo wengi wetu hasa wapenzi na mashabiki wa soka tulidhani itakuwa ni mkombozi katika soka yetu inayopoteza ladha?

    GAZETI LA MWANANCHI:
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAPI INAELEKEA LIGI KUU YETU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top