| ||
Yanga imeyumba katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kujikuta ikiishia nafasi ya tatu huku Simba ikiipora ubingwa na Azam Fc ikishikilia nafasi ya pili.
Gazeti la Mwanaspoti leo limeandika kwamba, wamefanikiwa kuona ripoti mbalimbali zilizoandikwa na madaktari waliokuwa na Yanga kwa vipindi tofauti msimu mzima zimebainisha kwamba usajili wa kiholela bila kufanya vipimo vya awali umechangia matatizo hayo ya kiafya.
Madaktari hao wameonyesha kuwa matatizo makubwa yaliyojitokeza kwa asilimia kubwa ni kuchanika kwa msuli mgumu (ligaments), nyama, kuvimba kwa vifundo vya miguu na maungio ya mifupa.
Matatizo mengine ni pamoja na afya ya akili (matatizo ya kisaikolojia)na ulevi wa kuvuta sigara na unywaji wa pombe.
Kwa mujibu wa ripoti hizo ambazo zimeushutumu uongozi kwa kutokuwa makini wakati wa usajili, zimeeleza kuwa asilimia kubwa ya wachezaji hao kama uchunguzi wa kitaalamu ungefanyika awali baadhi yao wasingesajiliwa kwavile wangelazimika kukaa nje muda mwingi kwa matibabu.
Kuhusu Gumbo, habari za ndani zinasema kuwa madaktari wameeleza kuwa ana tatizo ambalo linahitaji uangalizi wa kitaalamu.
Sehemu ya ripoti hizo inasema kuwa ; "Tatizo la Gumbo si la kudumu bali linaweza kutokea anapokuwa mchezoni hususani anapokuwa anachinja mipira(kupiga daglish au kupiga mipira outer). Tatizo hilo humfanya asiweze kabisa kuendelea na mchezo kwa siku husika na humchukua takribani dakika 45 hadi saa 2 kupoa bila kutumia dawa. Kimsingi mchezaji huyu kwa hali ya Tanzania anaweza kutumika chini ya uangalizi wa daktari kwa vile msuli kamba unaounganisha mifupa kwenye maungio unaomsumbua imesababishwa na kulegea kwa msuli kamba (subluxation of ligament) na hivyo kuwa inatoka katika sehemu yake pindi kiungo hicho cha goti la kulia kinapowekwa katika mkao tofauti."
Uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia 30 ya wachezaji ambao ni wale muhimu na wa kutegemewa kwenye kikosi cha kwanza wakiwemo wote wa kigeni wana wamegundulika kuwa na matatizo ya kiafya ambayo kwa kiasi fulani yamechangiwa na matunzo mabovu ya kitaalamu katika mazingira waliyoyakuta ndani ya Yanga.
Katika ripoti hizo mbalimbali uongozi umeshauriwa kuwa na timu ya afya yenye ujuzi na vyeti ambayo itapima afya za wachezaji kabla na wakati wa mapumziko ya ligi ili kudurusu afya zao na kisha kujua tatizo kabla ya kumuondoa kabisa mchezoni kwa matibabu.
Wataalamu hao kwa upande mmoja wameulaumu uongozi kwa kutowaamini wanataaluma wanaowaajiri hususani madaktari kwenye kufanya maamuzi na pia kuboresha miundo mbinu ya gym na sehemu ya kuogelea kwenye jengo la klabu kukabiliana na matatizo ya wachezaji
0 comments:
Post a Comment