// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAARABU KUCHEZESHA STARS NA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAARABU KUCHEZESHA STARS NA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 15, 2012

    WAARABU KUCHEZESHA STARS NA IVORY COAST


    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeteua marefa kutoka Tunisia na Misri kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
    Mpuliza kipyenga atakuwa Slim Jedidi wakati msaidizi wake namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia na msaidizi namba mbili atakuwa Sherif Hassan kutoka Misri na wa akiba Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
    Mtathmini wa marefa atakuwa Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamisaa atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.
    Wakati huo huo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya TFF, utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu.
    Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
    Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).
    Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata.
    Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi, Kenya.
    Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAARABU KUCHEZESHA STARS NA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top