// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 15, 2012

    VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA


    Ruud van Nistelrooy
    ALL OVER ... Ruud van Nistelrooy has quit
    Published: 14th May 2012

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy amestaafu soka.

    Van Nistelrooy mwenye umri wa miaka 35, amekuwa katika wakati mgumu tangu amejiunga na Malaga akitokea Hamburg msimu uliopita, akifunga mabao matano tu katika mechi 32.
    Licha ya ukame wake wa mabao, ameisaidia klabu hiyo ya Hispania kumaliza ndani ya Top-Four ya La Liga kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao na kufuzu kucheza Ligit ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
    Mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi, alisema: “Jana ilikuwa siku yangu ya mwisho katika soka ya kulipwa. Nilitaka kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini ni wakati wa kuondoka.
    “Nimefikia kwenye kiwango cha mwisho cha ubora na siwezi kucheza kwa kiwango kinachotakiwa. Siwezi kuagwa vizuri zaidi ya hivi,"alisema.
    Van Nistelrooy alianzia soka nyumbani kwao na klabu ya Den Bosch kabla hajahamia Heerenveen na PSV Eindhoven, ambako alijijengea jina.
    Baada ya kutwaa kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu Uholanzi, Eredivisie Golden katika misimu ya 1998/99 and 1999/2000, alichukuliwa kwa bei mbaya na vigogo wa Old Trafford.
    United ilimsajili Van Nistelrooy bila ya kujali kama alikuwa majeruhi wakati huo, akisumbuliwa na maumivu ya goti aliloumia mazoezini.
    Van Nistelrooy alilipa fadhila kwa kolcha huyo Mscotland, kwa kumfungia mabao 150 katika mechi 219 ndani ya misimu mitano ya kuitumikia Manchester na kuipa taji msimu wa 2002/03.
    Baadaye aliuzwa Real Madrid mwaka 2006, ambako alifunga mabao 53  katika misimu miwili, akiiwezesha Real kutwaa mataji mawili mfululizo ya La Liga.
    Lakini akaumia tena na akaukosa karibu msimu wote wa 2008/09 na kuzidiwa kete na akina Raul, Gonzalo Higuain na Karim Benzema katika msimu uliofuata.
    Alitimkia Hamburg ya Ujerumani alikocheza miezi 18 kabla ya kurejea Hispania kuchezea Malaga.
    Van Nistelrooy pia amefunga mabao 35 katika mechi 70 za timu ya taifa ya Uholanzi— ikiwemo aliyofunga kwenye Euro 2004, Kombe la Dunia 2006 na Euro 2008 — na mfungaji bora wa pili kihistoria katika Ligi ya Mabingwa, akiwa ametikisa mabao 54 katika mechi 81.
    Mechi yake ya mwisho ilikuwa kati ya timu yake, Malaga ambayo walishinda 1-0 dhidi ya Sporting Gijon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VAN NISTELROOY ATUNDIKA DALUGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top