Twiga Stars |
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza ‘vibaya
kidodo’ kampeni za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa
wanawake, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni hii mjini Addis Ababa na wenyeji,
Ethiopia.
Twiga sasa inahitaji ushindi wa 1-0, Juni 16, katika mchezo
wa marudiano mjini Dar es Salaam, ili kukata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa
mara ya pili mfululizo, Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane
katika historia ya michuano hiyo.
Wakati huo huo: Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).
0 comments:
Post a Comment