TATIZO
KUTOTAMBUA KIINI CHA TATIZO!!!
Napenda kuwasalimu wapenzi wa michezo wote nchini hasa hasa mchezo wa soka.
Ni jambo lisilopingika kwamba watanzania wengi
wanaupenda mchezo wa soka. Ndio maana hata viongozi wa soka wa nchi kadhaa jirani zetu wamekiri
hilo,mathalani tumeshuhudia kombe ka Chalenji likifanyika mara kwa mara nchini
Tanzania kuliko nchi nyingine ya afrika Mashariki. Sababu kuu ambayo imekuwa
ikielezwa ni washabiki kuwa wengi na udhamini mathubuti.
Hebu turudi kwenye mada yetu ambayo ninataka
kuiongelea. Ni kweli kwamba watanzania wengi wanapenda soka. Lakini pamoja na
mapenzi haya kuna tofauti kubwa kati ya Tanzania na jirani Zetu mathalani Kenya,Uganda,Rwanda,na
Burundi katika swala la Kufadhili na kupenda timu mbalimbali katika Ligi zao. Tumeshuhudia
katika ligi kuu ya nchi hizi Klabu Bingwa imekuwa ikibadilikabadilika. Hii na
tofauti na hapa kwetu ambapo tumeshuhudia ubingwa ukichukuliwa na Simba na
Yanga tu. Ni kweli kwamba Mashabiki wengi wa Tanzania wamejiainisha zaidi kwa
Simba na Yanga hii ina maana kwamba mashabiki wengi na wafadhili wengi
wameegemea zaidi katika vilabu hivi viwili. Jambo hili si baya. Tatizo hapa ni
kwamba kutokana na Wengi wa wafadhili kusaidia Yanga na Simba Vilabu Vingine
vya mitaani ambavyo ama si vya Makampuni au Majeshi vimeshindwa kupambana
kifedha na Timu hizi kubwa hatimaye zimeishia kufanya usajili duni wa wachezaji
wa kiwango cha chini kiasi cha kuzifanya
zimalize ligi ama zikiwa mkiani ama kushuka kabisa baada ya kuwa zimepanda si
muda mrefu.
Katika hali kama hii ni vyema basi washikadau wa soka
letu wakafikiria pia kuzisaidia timu hizi. Nampongeza ndugu yetu Bakresa
aliyeamua kuanzisha timu yake ya Azam. Mtakubaliana nami kwamba timu hii walau
imetoa ushindani thabiti kwa Simba na Yanga kiasi hata cha kuifanya mpaka dakika hii iwe katika
nafasi ya pili katika msimamo wa ligi na kujihakikishia nafasi mojawapo ya
kuiwakilisha nchi katika mechiza kimataifa mwakani.
Sasa hebu tuangalie upande wa pili wa hoja
zinazotolewa na wadau kuhusu soka letu. Mathalani kuongezeka kwa timu za
majeshi katika ligi yetu. Kwa upande wangu mimi naona hili ni jambo jema sana
tena linaleta changamoto. Mathalani pamoja na kutochukua ubingwa timu za
majeshi zimekuwa zikitoa ushindani kiasi Fulani kwa Simba na Yanga kuliko timu
za kiraia. Lakini kwa upande mwingine nataka wadau wafahamu kabla ya kukosoa
uwepo wa timu za majeshi ama kuzidi kwa timu za majeshi katika ligi yetu
wajiulize chanzo nini?.
Kama
nilivyotangulia kusema hapo mwanzoni swala la timu za mitaani kutokuwa na
wafadhili na wapenzi wa kutosha ndio chanzo kikubwa cha kuwa na timu nyingi za
jeshi katika ligi. Siku za nyuma niliwahi kusoma katika gazeti la mwanaspoti
tarehe 24-27 mwezi wanne hoja iliyoandikwa na mchambuzi wangu mahiri Bwana Eddo
Kumwembe. Habari hii ilikuwa na kichwa cha habari ‘’AMESHUKA AFANDE MMOJA
KAPANDA MWINGINE’’ Akimaanisha kashuka
Polisi Dodoma wamepanda Mgambo JKT,Tanzania Prison na Polisi Morogoro!.
Mchambuzi aliendelea kushauri kwa mfano alisema kwa nini kusiwe na timu moja
mathalani Jeshi la Polisi,Magereza, JKT na Jeshi la wananchi kuwa na timu moja
moja kuliko kuwa na nyingi? Ati ili kuwa na Timu imara?. Niliwahi pia kusoma
habari nyingine kwenye RAIA MWEMA yenye kichwa ‘’ TUSIPOKUWA MAKINI LIGI
ITACHEZWA MAKAMBINI’’ habari ya Mwandishi Ezekiel Kumwaga. Mimi binafsi si
afiki mawazo ya waandishi hawa kama hayatakuwa yanaanisha kiini cha tatizo na
njia ya kuondoa tatizo .
Mathalani tumekuwa na kambi za Jeshi katika Mikoa
mbalimbali sasa huwezi sema kuwe na timu mfano labda JKT Ruvu tu ambayo ipo Dar
es salaam ndo iwakilishe JKT zote Tanzania !!! Wakati katika mikoa mingine
zipo!!. Si zani kama hii ni sahihi. Kwa sababu kwa mtu yeyote anayefahamu muundo
wa Jeshi huwa na Timu za michezo mbalimbali ukiwemo soka. Na kila Kambi ya
Jeshi ingependa ipate timu yake ya kuiburudisha sasa kama JKT itakuwa ya Dar es
salaam tu je Wanajeshiwa wa mikoa mingine watapata wapi burudani ya soka? Au
wataona wapi soka??.
Pili wazo kwamba timu za majeshi ni za mwajiri mmoja
halina tija kwa kuwa swala kubwa niburudani na pia hakuna sheria ambayo
inakataza timu za majeshi kushiriki ligi ati kwa kuwa ni za mwajiri mmoja
ingekuepo basi ningeafiki wazo la mdau. Swala kuu hapa tujiulize ni kwanini
tumefikia hapa? Kwa nini timu za kiraia
mathalani zile zilizoleta ushindani wa kiwango cha juu miaka iliyopita
hazipo ama kwa nini zinazidi kupotea? Kwa mfano Ipo wapi Majimaji Songea ? Wapo
wapi African Sports?, Wapo wapi Pamba ya Mwanza? Wapo wapi Ushirika ya Moshi?
Wapo wapi Tukuyu Stars? Wapo wapi Lipuli n.k ? Kwa nini zilishuka? Kwanini
hazirudi ligi kuu? Tukiweza kutengua ni kwa nini timu hizi zimeshuka na zinashindwa
kurudi nazani tutaweza kutatua tatizo.
Ushauri wangu sasa kwa wadau wenye mawazo kama ya
Wachambuzi wangu ni bora wakahamasisha
watanzania mbalimbali wenye uwezo wakafanya kama M. Bakresa kwa kuunda ama
kufazili timu ili zilete ushindani kwa Yanga na Simba na si Kulalamikia uwepo
wa Timu za majeshi katika ligi yetu. Tukifanikiwa katika Hili basi hakuna shaka
tutakuwa tumewaondolea dukuduku ndugu yangu Eddo Kumwembe na Ezekiel Kumwaga
IMEANDIKWA NA MDAU WA BIN ZUBEIRY, mpendasoka Charles. Wasiliana naye kwa email;
charlesnuru@yahoo.co.uk
0 comments:
Post a Comment