KLABU ya SuperSport United ya Afrika Kusini jana iliwafunga Mamelodi Sundowns waliomaliza mechi wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja, mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Orlando na kutwaa Kombe la FA la Afrika Kusini kwa mara ya tatu.
Beki wa kati wa Sundowns Clayton Daniels alitolew3a nje kwa kadi nyekundu dakika ya 19, baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa SuperSport, Kermit Erasmus kwejnye eneo la penalti.
Mbali na hundi ya dola za Kimarekani 720,000, kwa kutwaa taji hilo, SuperSport timu aliyowahi kuchezea kiungo wa zamani wa Simba SC, Suleiman Matola imejikatia tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani, michuano ambayo kwa Tanzania, mwakilishi wake ni Azam FC.
0 comments:
Post a Comment