// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TIBAIGANA AZIRUDISHA UWANJANI AZAM NA MTIBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TIBAIGANA AZIRUDISHA UWANJANI AZAM NA MTIBWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 03, 2012

    TIBAIGANA AZIRUDISHA UWANJANI AZAM NA MTIBWA

    Wachezaji wa Azam
    KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shiriksho la Soka Tanzania (TFF) imeamuru mchezo kati ya Azam FC uliovunjika zikiwa zimesali dakika chache, timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam urudiwe.
    Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka kwenye kikao cha Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Kamanda Mstaafu, Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Alfred Tibaigana kilichofanyika jioni ya leo Dar es Salaam, zimesema kwamba mchezo utarudiwa kwa sababu imebainika makosa yalikuwa ni ya waamuzi na si Mtibwa.
    Kama imebaini waamuzi hawakufuata kanuni za kusubiri kwa dakika 10, wakati wachezaji wa Mtibwa Sugar wamegoma kabla ya kumaliza mchezo.
    Matokeo yanamaanisha, Azam sasa itabaki na pointi 53 na mechi mbili, ukiacha hiyo ya marudio na Mtibwa, pia watacheza na wakata miwa wengine, Kagera Sugar.
    Ikumbukwe mchezo huo ulivunjika baada ya Mtibwa kugomea penalti, waliyopewa Azam wakidai si halali.
    Simba inaendelea kuongoza ligi kwa pointi zake 59 na imebaki na mechi moja tu dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumamosi ambayo wanahitaji sare tu kujihakikishia ubingwa.
    Azam ikiwa na wastani mzuri zaidi wa mabao, huku ikipigania ushindi kwenye mechi zake mbili za mwisho, pia inaiombea duwa m baya Simba ifungwe na Yanga ili ibaki na pointi 59 ilizonazo- halafu bingwa wa Ligi Kuu msimu huu, aamuriwe kwa mabao kama msimu uliopita.
    Msimu uliopita walikuwa ni Yanga ambao waliipiku kwa wastani wa mabao Simba na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
    Kwa upande mwingine, kurudiwa kwa mchezo huu ni pigo pia kwa klabu ya African Lyon, ambayo ilikata rufaa kupinga maamuzi ya awali ya Kamati ya Ligi Kuu, kuipokonya Mtibwa pointi kwa kosa la kugomea mchezo, pasipo kuishusha daraja kama kanuni inavyosema.
    Aidha, hata kitendo cha Lyon kuikatia rufaa kwa kucheza nayo bila kulipa ya Sh 500,000 walizotozwa na Kamati ya Ligi nacho hakina nguvu tena, kwa kufutwa kwa matokeo ya mchezo huo kunafuta na adhabu pia.
    Ligi Kuu msimu huu inaonekana dhahiri kuyumbishwa na maamuzi ya Kamati ya Ligi Kuu, kwa kukosa msimamo wa kufuata kanuni maalum zilizowekwa kwa ajili ya Ligi Kuu na wakati mwingine eti kuamua kwa kufuata kanuni za FIFA.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIBAIGANA AZIRUDISHA UWANJANI AZAM NA MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top