TIMU za soka za taifa zaTanzania, Taifa Stars na Malawi ‘The Flames’ leo zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimisha sare ya 0-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni mahususi kwa timu hizo kujinoa kwa ajili ya mechi zake za mchujo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia Juni 2, ambapo Stars itakuwa Ivory Coast, huku Malawi itakwaana na Kenya ambapo zote zitacheza ugenini.
Mpaka mwamuzi wa mchezo huo Oden Mbaga anapuliza filimbi ya mwisho, hakuna rimu iliyofanikiwa kutikisa nyavu za mwezake.
Stars:Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Wazir Salum/Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondan, Shaban Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Haruna Moshi ‘Boban’na Mwinyi Kazimoto.
Malawi:Simplex Nthala, Limbikani Mzava, Moses Mvula, Foster Namwela, James Sangala, Joseph Kamwendo, Frank Banda, Dave Banda/Jimmy Zakazaka, Zicco Mkanda/Amadu Ally, Robin Ngalande na Russell Mwafulirwa/ Ndaziona Chatsalira.
0 comments:
Post a Comment