Simba |
Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Shandi, penalti za Shandy zilifungwa na Razak Yakubu,Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun Malik,Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu
na kipa Abdulrahman Ali.
Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu,
Salum Machaku, Emanuel Okwi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi
Kazimoto na Amir Maftah.
Eltigani alikosa kwa upande wa Shandy
wakati Mafisango na Kaseja walikosa. Aliyeihakikishia Simba kutolewa alikuwa
ni Nahodha Kaseja, ambaye alikosa penalti ya 10.
Shandy waliingia kwenye mchezo wa leo,
wakiwa nyuma kwa 3-0 kutokana na ujshindi wa SImba kwenye mechi ya kwanza, Dar
es Salaam.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyokuwa
imeona lango la mwenzake na hiyo ilijenga matumaini kwamba, SImba itasonga
mbele, lakini kipindi cha pili mambo yalibadilika mno.
Mabao mawili ya Fareed Mohamed katika za 46
na 64 na lingine la Hamouda Bashir dakika ya 50, yaliisaidia Al Ahly Shandy
kushinda 3-0 na kufanya sare ya jumla ya 3-3, baada ya dakika 180 za mechi
mbili.
Lawama zote zimuendee beki Victor Costa kwa
kufungisha mabao mawili- hususan la pili na la tatu ambalo dhahiri yalitokana
na ‘ubishoo’ wake usio na maana.
Hii inahidhirisha mchezaji huyo aliyepangwa
kwa dharula leo, kocha Milovan Cirkovick alikuwa hakosei kutompanga kwani leo
ameigharimu timu na haijulikani kwa nini apangwe yeye badala ya Obadia Mungusa.
0 comments:
Post a Comment