// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERENA AMTANDIKA MCHEZAJI BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERENA AMTANDIKA MCHEZAJI BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 14, 2012

    SERENA AMTANDIKA MCHEZAJI BORA


    13 Mei, 2012 - Saa 17:52 GMT
    Serena Williams
    Serena Williams
    Serena Williams amemshinda mchezaji anayeshikilia namba moja duniani Victoria Azarenka 6-1 6-3 kushinda mashindano ya Madrid Open kwa mara ya kwanza.
    Hii ni mara ya kwanza kwa Serena Williams kushiriki mashindano barani Ulaya msimu huu na mchezaji huyo ambaye ameshuka hadhi hadi namba sita alimiliki mchezo msima kwa seti zote mbili.
    Mchuano uliendelea kwa zaidi ya saa moja ambapo Mmarekani aliibuka mshindi na kuthibitisha kiwango chake cha uchezaji kua bora akitazamia kushiriki mashindano ya Ufaransa, French Open yanayoanza Mei 27.
    Azarenka
    Victoria Azarenka
    Ushindi pekee wa Azarenka mbele ya Williams ulitokea mwaka 2009 kwenye fainali ya mashindano ya Miami, lakini hiyo ni historia ambayo Mmarekani hakutaka kukumbushwa.
    Mashindano haya ya Madrid Open ni ya pili mfululizo ya vumbi kwenye ratiba ya WTA kwa Williams kushinda, siku chache baada ya kushinda ya huko Charleston
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENA AMTANDIKA MCHEZAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top