Published: 56 minutes ago
KENNY DALGLISH amefukuzwa na Liverpool baada ya miezi 16 ya kufanya kazi.
Licha ya kuiongoza klabu hiyo, kutwaa Komeb la Ligi maarufu kama Carling Cup na kucheza fainali ya Kombe la FA, ambako ilifungwa kwa utata na Chelsea, lakini kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu kumemponza.
Ikiwa imemaliza katika nafasi ya naneLigi Kuu- hiyo ni kinyume cha matarajio ya klabu hiyo, kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Liverpool imemaliza msimu ikiwa na pointi 52 —ambazo ni chache zaidi kihistoria katika ushiriki wao kwenye Ligti, wakizidiwa kete na wapinzani wao wa Merseyside, Everton.
Wakali hao wa Anfield pia walishinda mechi chache mno kihistoria msimu huu, 14, tangu msimu wa 1953-54 na wamfunga mabao machache zaidi (47) tangu msimu wa 1991-92.
Wamiliki wa timu pia hawakufurahishwa na jinsi alivyokuwa akimchukulia Luis Suarez .
Dalglish alitua Liverpool akirithi mikoba ya kocha wa sasa wa England, Roy Hodgson Januari mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment