Rachel kulia akiwa na mtoto Cessa enzi za uhai wake |
MWILI wa aliyekuwa Mhariri wa Habari za
Michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa unatarajiwa kuagwa kesho
Jumatatu Mei 14, 2012 saa nne kamili asubuhi katika Kanisa la Anglikana,
Ubungo, ambalo lipo nyuma ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msemaji wa familia, Alex
Chimila, taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitaanza saa 4:00 asubuhi na
kumalizika saa 6:00 mchana, tayari kwa msafara wa kwenda kuzika katika Makaburi
ya Tegeta A, Goba, jijini Dar es Salaam.
Alisema uamuzi wa kuaga mwili kwenye eneo
hilo una lengo la kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa ya kushiriki
kwenye tukio hilo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando ametoa wito kwa waandishi wa
habari za michezo na wadau wengine wa michezo na burudani kujitokeza kwa wingi
asubuhi kwenda kumuaga mpendwa wetu.
Rachel alifariki dunia usiku wa kuamkia
juzi, kwenye hospitali ya Mwananyamla, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa
matibabu.
0 comments:
Post a Comment