// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); POULSEN AWATEMA NYOTA WAWILI SIMBA SAFARI YA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE POULSEN AWATEMA NYOTA WAWILI SIMBA SAFARI YA IVORY COAST - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 31, 2012

    POULSEN AWATEMA NYOTA WAWILI SIMBA SAFARI YA IVORY COAST

    Wachezaji wa Taifa Stars wakiingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam alfajiri ya leo tayari kwa safari ya Ivory Coast.


    NYOTA wa klabu ya Simba, beki Said Nassor 'Chollo' na kiungo Haruna Moshi 'Boban' wameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoondoka alfajiri ya leo Dar es Salaam kwa ndege ya Kenya Airways kwenda Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayochezwa Juni 2 mwaka huu.
    Kocha Kim Poulsen alisema wakati timu hiyo ikiondoka wachezaji hao ni majeruhi ndio maana kawaacha. Wachezaji walioondoka na timu i Nahodha Juma Kaseja, Nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.
    Boban na Chollo wanaungana na wachezaji wengine wawili, waliobaki kutokana na kuwa majeruhi, mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari.
    Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba
    Viongozi waliofuatana na timu hiyo ni Kocha Mkuu Kim Poulsen, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
    Msafara huo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori wakati naibu kiongozi wa msafara ni Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir Haji.
    Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliagwa leo (Mei 30 mwaka huu) na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye aliwataka wachezaji hao kwenda kuiwakilisha vizuri Tanzania kwenye mechi hiyo.
    Hafla hiyo ya kukabidhi Bendera ya Taifa pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, Rais wa TFF, Leodegar Tenga na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
    Mechi itachezwa kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
    Kiungo Haruna Boban, enzi zake akicheza Ulaya, Geffle FF ya
    Ligi Kuu Sweden, kabla ya kurejea kwenye soka ya madafu
    Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
    Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.
    Stars itarajea nyumbani Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Gambia itakayofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POULSEN AWATEMA NYOTA WAWILI SIMBA SAFARI YA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top