Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya

VICHWA VYA HABARI VYA UBINGWA WA MAN CITY ENGLAND:
"Miracle Manc!" - the Sun
Manchester City's coaching staff
City yamaliza ukame wa ubingwa wa Ligi Kuu wa miaka  44


"We won it in Fergie time" - the Sun
"Foot of God" - Daily Mirror
"Wincredible - most amazing title clincher ever" - Daily Star
"Paradise City" - Guardian
"Over the blue moon" - Daily Express
"Mancini's crazy gang make every last second count" - The Times
"Miracle men - City end 44-year title hoodoo with most dramatic finale in history" - Daily Telegraph

UNITED, SPURS ZAGOMBEA BEKI LA UFARANSA

Manchester United na Newcastle zinaandaa uhamisho wa dau la pauni Milioni 6.5 kwa beki wa kulia wa Ufaransa, Mathieu Debuchy baada ya Lille kusema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ataruhusiwa kuondoka.
Gwiji wa Hispania, Raul ameondoka klabu ya Schalke ya Ujerumani, ambako aliibuka kipenzi cha mashabiki akitupia mipira 27 nyavuni katika mechi 63 za Bundesliga, akisaini klabu ya Al Sadd ya Qatar.
Derby imekataa ofa ya pauni Milioni 1.2 kutoka Burnley kwa ajili ya beki wao, Jason Shackell, mwenye umri wa miaka 28.
Mchezaji anayewaniwa na Liverpool, Rasmus Elm amewaonya Wekundu hao kwamba fikra ziko mbali na kuihama klabu yake, AZ Alkmaar ya Uholanzi m simu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 24amesema "anajisikia vizuri AZ".
Manchester United striker Dimitar Berbatov
Berbatov alitua Man Utd akitokea Tottenham 2008


Middlesbrough inavutiwa na mchezaji wa Portsmouth, Luke Varney, mwenye umri wa miaka 29, na mshambuliaji huyo anaweza kupigwa bei kwa dau la pauni 375,000.
Liverpool pia inataka kutoa ofa nyingine kwa mshambuliaji aliyefulia wa Manchester United, Dimitar Berbatov, ambaye amecheza mechi tano tu msimu huu wa Ligi Kuu ya England.
Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy amesema kwamba hakuna kati ya wachezaji wao tegemeo, atakayeondoka White Hart Lane msimu huu.
Everton inataka kumsajili kipa wa Olympiakos, raia wa Hungary, Balazs Megyeri ili akampe ushindani Tim Howard Uwanja wa Goodison Park. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake, anaweza kuwagharimu pauni 800,000.
Cardiff na Ipswich inafanya majadiliano na kipa Joe Lewis, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anajiandaa kuondoka Peterborough kama mchezaji huru.

MANCINI ALIANZIA KANISANI

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini alikwenda kusali kanisani na wachezaji wawili kabla ya City kutwaa ubingwa jana, kiaina yake.
Kiungo wa Manchester United, Paul Scholes, mwenye umri wa miaka 37, amefungua milango ya mazungumzo na kocha wa timu ya taifa, Roy Hodgson juu ya kurejea kwenye soka ya kimataifa.
Paul Scholes
Paul Scholes alistaafu timu ya taifa 2004


Sir Alex Ferguson ametoa ujumbe wa wasiwasi kwa mashabiki wa Manchester United, kwamba Nahodha Nemanja Vidic atakosa ziara ya kujiandaa na msimu mpya.
Hull City 'imemtongoza' kocha wa zamani wa Leeds na Sheffield United, Kevin Blackwell ili awe kocha wao mpya. The Tigers wamemfukuza Nick Barmby wiki iliyopita.