Hii ndiyo mechi iliyokamilisha maisha ya Fusso Jangwani. kama anavyoonekana kulia akifunga tela kwa Okwi wa Simba Mei 6, mwaka huu, Yanga ikila 5-0, tatu zikipitia kwake. |
KLABU ya Yanga imewatema rasmi katika
usajili wake, washambuliaji Davies Mwape kutoka Zambia na Kenneth Asamoah wa
Ghana, wakati Nahodha Nsajigwa Shadrack 'Fusso' anaweza kutolewa kwa mkopo sawa na Abuu
Ubwa na Bakari Mbega.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka
Kamati ya Ufundi ya Yanga, iliyo chini ya Mwenyekiti wake, Mohamed Bhinda ni
kwamba benchi la ufundi limependekeza wachezaji hao waachwe kwa sababu hawana
msaada kwenye timu.
“Ambao mikataba yao imeisha tunawaacha moja
kwa moja, ambao bado wana mikataba itabidi tuwatoe kwa mkopo,”kilisema chanzo
kutoka Kamati ya Ufundi.
Aidha, chanzo kimesema kwamba msimu huu,
Yanga itaelekeza nguvu zake kwenye kikosi cha pili zaidi- kuhakikisha
wanawekeza zaidi huko ili kuvuna wachezaji bora.
“Tutasajili timu imara ya kikosi cha kwanza
kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, lakini pia tutahakikisha tunawkeza sana kwenye
timu B,”kilisema chanzo hicho.
Wakati Nsajigwa alikuwa uchochoro Mei 6, mwaka huu Yanga ikifungwa 5-0 na SImba, Asamoah na Mwape wameshindwa kuifungia mabao ya kutosha timu hiyo katika Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment