Published: Today at 17:13
ROBERTO MANCINI anataka fedha zaidi za usajili ili kuifanya Manchester City iwe kama Barcelona.
Mancini amesema anaweza kuleta taji la Ulaya kwa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya England — kama atapata fungu kubwa la usajili kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao.
City imetumia fedha nyingi kusajili nyota kama Yaya Toure, Edin Dzeko, Carlos Tevez na Sergio Aguero.
Lakini kocha Mancini amesema kwamba kuleta mafanikio zaidi City iwapo tu atapewa fungu lingine kubwa la usajili.
Mtaliano huyo alisema: “Barcelona na Real Madrid kila mwaka wananunua wachezaji wawili au watatu na wanatumia fedha nyingi.
“Nafikiri kwa Manchester City itakuwa kama hivyo.
“Tunahitaji kuimarika. Tunahitaji kuwa na nguvu za kucheza Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu.”
0 comments:
Post a Comment